Na Chrispin Kalinga
Njombe
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Ndg, Edwin Swalle na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Ndg, Msafiri Mpolo wametangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi Leo.
Ndg, Edwin Swalle na Ndg, Msafiri wametangaza uamuzi huo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe, na kupokelewa na Viongozi wa CCM wakiwemo Madiwani kutoka Kata mbalimbali Wilayani Njombe waliokuwa wakiendelea na Kikao chao na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, Ruth Msafiri.
Licha ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Edwin Swalle ni Wakili Msomi na alikuwa Mwanasheria wa Chama hicho pia ni Miongoni mwa Wagombea nafasi ya Ubunge Mwaka 2015 katika Jimbo la Lupembe kupitia CHADEMA akishindana na Mbunge wa Jimbo hilo aliyeibuka Mshindi kupitia CCM Mhe, Joramu Hongoli.
Akitangaza Kuihama CHADEMA na Kujiunga na CCM Wakili Swalle amesema hana Chuki na Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe, Joramu hongoli badala yake atatumia Taaluma aliyonayo kuhakikisha anamsaidia Mbunge huyo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli katika Kutekeleza Majukumu yao.
“Bahati Pekee ambayo Tanzania tumeipata ni hii ya kumpata Rais Magufuli, hatakiwi kutukanwa bali anahitaji kuungwa Mkono, haitaji Kukosolewa ila anahitaji kulindwa na kushauriwa ili azidi kututumikia Watanzania, tumeona Soko la Kisasa, Stendi kubwa na Hospitali kubwa Imejengwa Njombe ” Bw, Swalle.
Hatahivyo amesema Ameamua Kujiunga na CCM bila kushauriwa na Mtu yeyote ni Baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho unaofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli ambae ameamua kuirudisha Heshima ya Chama Cha Mapinduzi Nchini.
“Nilikuwa Nchini Afrika Kusini ilipotua Ndege ya Tanzania Wenzetu kule wanasema Magufuli anaingia Nchini nikatafakari sana na kuona kweli Rais
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking