Dinsdag, Mei 17, 2022



Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Waziri Waziri Kindamba jana Mei 12, 2022 alitembelea kiwanda cha muwekezaji mkubwa wa Parachichi Mjini Makambako katika mkoa wa Njombe kinachojulikana kwa jina la AvoAfrica.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pamoja na mambo mengine alikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na muwekezaji wa kiwanda hicho haswa katika utaratibu mzima wa uchakataji wa Parachichi hadi hatua ya mwisho.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri Kindamba wakati akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi wa maeneo hayo alisema kuwa;

Ndugu wananchi wa Mkoa wa Njombe na Watanzania wote, nitumie nafasi hii kuwahakikishia wawekezaji wote kuwa, Njombe ni sehemu salama ya uwekezaji na tunawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza katika Mkoa wa Njombe katika sekta ya Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Utalii bila kusahau Madini kule Ludewa_ ,*

Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba aliongeza kwa kusema kuwa;

Muwekezaji yeyote atakayekuja kuweka Mtaji wake Njombe tupo tayari kuwalinda kwa wivu mkubwa ili vijana wetu waendelee kupata Ajira.

Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa alisema kuwa Wawekezaji wanapokuja kuwekeza Njombe Serikali inapata faida kwa ulipwaji wa Kodi kutoka kwa wawekezaji hao lakini pia Wananchi wananufaika na mambo mbalimbali ikiwemo Ajira, mzunguko wa Biashara n.k.

Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

 

Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-

  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.