Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonekana kuvuruga zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuahidi kumchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria ya nchi ikiwemo kulipia faini kiasi cha fedha kisichopungua Ml.1, Jela miezi sita au vyote kwa pamoja.
Kauli hiyo ameitoa katika mikutano ya kutoa elimu juu ya zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi iliyofanyika katika kata ya Luilo, Luhuhu pamoja na kata ya Manda.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Isaac Ayengo amesema adhabu hizo zipo kwa mujibu wa sheria ya sensa kifungu namba 43(3) ambacho kinaeleza makosa ambayo raia hapaswi kuyafanya .
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking