Picha na France malekela
wa kwanza kushoto kwako ni mkurungenzi mkuu wa chuo
Wa pili aliye vaa hereni ni mwalimu chuo cha uandishi wa habari na anafundisha masomo ya uongozaji wa hotel za kimataifa
anaitwa Madam Tunu Eliya Kyando.
Huyu pia ni moja ya wafanyakazi wa hotel ya AGREEMENT iliyopo mkoani Njombe Ambaye anaitwa Evodia Patrick Chillumba anakahimu nafasi ya Meneja ambayo wanachuo hao wamefanya ziara .
Na hawa ni moja ya mchanganyiko wa wanafunzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari..
Huyu pia ni Chrispiny kalinga mwalimu wa mafunzo ya Udereva na News Writting.
Huyu pia ni Mwalimu wa Kompyuta anaitwa France Malekela
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utandazaji Eckros school of jounalism kilichopo mkoani njombe wamefanya ziara ya kimasomo katika hotel kubwa mkoani hapo.Hali kadhalika wanafunzi wa uandishi wa habari sambamba na wanafunzi wa mosomo mengine waliambatana nao katika ziara hiyo na kujifunza mambo mbalimbali yatakayo weza kuwasaidia kwenye maisha yao baada ya kumaliza masomo na kuanza maisha yao ya ajira na kujiajiri wenyewe.
Baadhi ya wanachuo hao wamezungumza na blog yetu ya Mubashara blog kuwa uwepom wa chuo hicho kimewasaidia kwa kiasi kubwa kwa kuwafundisha mambo mbalimbali ambayo hawakutegemea mengine hata kuyaona na wameyaona
Mwalimu wa chuo hiyo anafahamika kwa jina madam Tunu alizidi kuwasihi wanafunzi hao kuzingatia yale wanayo jifunza kwa vitendo katika maeneo yote ya ziara yao na akawasihi licha ya kumaliza masomo yao akawaeleza waandishi wa habari kuwa chuo hicho kinafundisha wanafunzi wa aina yoyote lengo ni kuokoa kizazi ambacho kinadharaulika kwa kuwapa elimu bora na yenye viwango
Akaongeza kwa kusema kuwa moja ya wanafunzi wengine wanapokelewa kwenye chuo hicho hawajui chochote ila kazi yao kubwa ni kuwatoa upumbavu na kuwaingiza werevu.
Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa Chuo hicho ERIKI MLELWA amezungumza na waandishi wa habari juu ya wanafunzi hao wanao tarajia kufanya mitihani yao ya mwisho mwezi Apr alisema kuwa anauhakika na vijana wao wa ngazi zote kuwa watafanya mitihani yao vizuri kwasababu wamenolewa vya kutosha
Pia mkuu huyo akazidi kusema kuwa anatumia nafasi hiyo kuwahamasisha walezi na wazazi kuwapeleka watoto wao katika chuo hicha kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa gharala nafuu ukilinganisha na vyuo vingine
Akaongeza kwa kusema kuwa chuo chake yeye kama mkurugenzi wa chuo hicho wanafunzi wake watakao fanya vizuri kwenye mitihani yao huwa anawatafutia ajira ndani ya nchi na nje ya nchi.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking