Sondag, Maart 31, 2019

FARAJA YA MAJI MKOANI NJOMBE IPO PEUPE


NJOMBE.
Image result for MAJI NJOMBE

NA AMIRI KILAGALILA

Mamlaka ya Maji Njombe Mjini NJUWASA imesema  kufuatia kuwepo kwa Changamoto ya Maji ndani ya Mji wa Njombe Serikali inamkakati wa Kujenga Mradi Mkubwa wa Maji kwa Ufadhili wa Serikali ya India ili kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata Huduma ya uhakika na ya kudumu.

Akiwa katika ziara ya kutembelea Vyanzo mbalimbali vya Maji vinavyohudumia mji Wa Njombe kikiwemo chanzo kipya cha Mto Hagafiro kinachotarajiwa kujengwa,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Njombe Mjini Mhandisi John Mtyauli amesema kuwa kuanzishwa kwa chanzo hicho kipya kutasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa Maji ndani ya mji huo ambao kwa sasa Asilimia kubwa huduma hiyo imekuwa ikitolewa kwa mgao.

Mhandisi Mtyauli ameweka wazi juu ya Uhalisia wa Mahitaji ya maji kwa sasa pamoja na kiwango cha maji kinachozalishwa na vyanzo  vilivyopo huku akikiri wazi kuwa Kiwango cha maji kilichopo  hakitoshelezi kulinganisha na idadi ya Watumiaji wa Huduma hiyo.

Itika Frank Mboka ni Maneja Biashara Mamlaka ya Maji Njombe mjini Ambaye anasema kuwa Mamlaka hiyo bado inaendelea kuhudumia wananchi licha ya Changamoto ya uchache huku akiwaomba wananchi kuendelea kuomba kuunganishwa na huduma hiyo.

Wananchi waishio Njombe mjini wanakiri kwamba changamoto hiyo ya maji inawakumba kwa kiwango kikubwa huku wakisema kuwa kuanzishwa kwa mradi huo wanaamini utakuwa mkombozi kwao.



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking