Vrydag, Maart 29, 2019

USHIRIKANA WAPAMBA MOTO MKOANI NJOMBE

Image result for USHIRIKINA
PICHA YA MTANDAONI.
NJOMBE.
TAARIFA  NA AMIRI KILAGALILA
Vitendo vya kishirikina vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wilayani Makete mkoani Njombe dhidi ya watumishi wanaopelekwa na serikali ama kwa wananchi wenzao vimekemewa vikali na mkuu wa wilaya ya Makete


Katika Mkutano wake na wananchi wa vijiji vya Mbalatse na Lupombwe mkuu huyo wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy amesema inashangaza mpaka sasa wananchi kuendelea kukumbatia vitendo hivyo ambavyo vinaitia aibu wilaya ya Makete ndani na nje ya wilaya hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya amewaomba viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo kwa kuwa moja ya kazi ya madhehebu ya dini ni kurekebisha mienendo ya waumini .

Mmoja wa mwananchi aliyekuwepo kwenye mkutano huo amewaomba wananchi wenzake wanaofanya vitendo vya kishirikina kuviacha kwa kuwa havina faida yeyote huku akielezea machungu aliyonayo ya kumzika wifi yake aliyefariki dunia kwa kukatwa mapanga kwa madai ya kujiusisha na vitendo vya kishirikina.

Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Godfrey Gogadi amesema ipo sheria ya uchawi hapa nchini na endepo itathibitika mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria na kuwaasa wananchi kuachana na vitendo hivyo ambavyo havina faida.
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking