Tarehe 31 Januari, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alizindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Rais Magufuli alikagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielekektronikia (e-Passport) ambayo pia ilianza kutolewa siku hiyo hiyo.
Passport hizo, zitamrahisishia mmiliki wake kuweza kupata huduma kirahisi zaidi katika nchi mbalimbali duniani ikilinganishwa na ilivyokuwa passport ya kawaida iliyokuwa inatumika hapo awali.
Wakati wa uzinduzi wa Passport hiyo, ilielezwa kuwa itapatikana kwa gharama ya shilingi 150,000/- ambayo ni tofauti na kiasi cha shilingi 50,000/- iliyokuwa ikitolewa kwa passport za zamani.
Tazama video hapa chini kujua hatua za kufuata ili kupata passport hii mpya ya kielektroniki.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking