Na. Dokta Mungwa Kabili …………….0744 000 473.
Pete ya Immoring ni pete ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana miongoni mwa wakaazi mbalimbali wa nchi za Afrika Mashariki na Ukanda wa Maziwa makuu kwa ujumla.
Nimekuwa nikipoea simu na jumbe kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka niwasaidie kujua namna pete ya Immoring inavyo fanya kazi pamoja na kuwaelesha uhusiano uliopo kati ya pete ya Immoring na suala zima la kusafisha, kuimarisha na kupandisha nyota, kutunza na kukinga nyota pamoja na mwili wa mwanadamu kwa ujumla Yafuatayo ndio majibu yangu.
Kabla sijaanza kuelezea kuhusu pete ya Immoring ni vyema nikaelezea nyota ni nini ? Ili kusudi unapotaka kujua uhusiano kati ya pete ye Immoring na masuala ya nyota, uwe unajua kinaongelewa kitu gani.
Nyota Ni Nini ?
Kwa lugha rahisi na nyepesi kabisa nyota ni ramani ya maisha ya mtu ambayo ameandikiwa na Mwenyezi Mungu.
Utajuaje Kama Nyota Ya Mtu Ni Safi Au Chafu ?
Utajuaje Kama Nyota Ya Mtu Ipo Juu Ama Ipo Chini ?
Utajuaje Kama Nyota Ya Mtu Ni Mbaya Au Nzuri ?
Kiashiria kikuu cha daraja ama hadhi ya nyota ya mtu ni namna mambo yanavyo muendea mtu huyo katika maisha yake. Au kwa njia rahisi kabisa unaweza kujua daraja ama hadhi ya nyota ya mtu kwa kuangalia kiwango cha riziki anayo ipata katika kazi ama shughuli zake za kila siku katika maisha.
Mtu mwenye nyota ya juu hata riziki yake itakuwa juu pia na Yule wa nyota ya chini riziki yake itakuwa chini pia kama ilivyo nyota yake.
Nyota Na Sehemu Kumi Na Mbili Za Mwili Wa Mwanadamu
Kwa kawaida ili mwanadamu aishi maisha ambayo watu wengine wakiyatazama wanaweza kukufuru na kusema mtu huyo kapendelewa, basi mtu huyo anapaswa kuwa na nyota 12 ambazo idadi yake ni sawa sawa na idadi ya sehemu kumi na mbili za mwili wa mwanadamu.
Katika ulimwengu wa kitabibu na kinyota mwili wa mwanadamu umegawanyika katika sehemu ndogo ndogo kumi na mbili ambazo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Sehemu hizi kuu mbili za mwili wa mwanadamu zinaunganishwa na kutenganishwa na kitovu. Sehemu ya kwanza ni sehemu ya juu kabisa ambayo inaanzia utosini hadi juu ya kitovu ilihali sehemu ya pili ni sehemu ya chini ambayo inaanzia chini ya kitovu hadi kwenye unyayo.
Sehemu ya juu imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo kila sehemu moja kati ya sehemu hizo tatu imegawanyika katika sehemu ndogo ndogo mbili mbili kila moja Vivyo hivyo sehemu ya chini nayo imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo nazo pia zimegawanyika katika sehemu ndogo ndogo mbili mbili kila moja.
Kila sehemu moja katika sehemu hizi kumi na mbili za mwili wa mwanadamu inawakailisha na kusimama badala ya nyota moja.
Sasa basi ili tuseme mtu Fulani nyota yake ipo juu, basi mtu huyo lazima awe amekamilisha idadi ya nyota zote kumi na mbili ambazo zinakamilisha idadi ya sehemu kumi na mbili za mwili wa mwanadamu.
Kwanini ni watu wachache tu ndio wanao kamilisha idadi ya nyota zote kumi na mbili?
Ni watu wachache sana duniani ambao wanakamilisha nyota zote kumi na mbili. Ni mtu mmoja katika maelfu . Sababu kuu ni fitna na dhulma zinazo fanywa na wachawi kwa kushirikiana na majini na masheitwani wachafu katika kushusha ama kuiba na kuzitumia nyota za watu mbalimbali.
Matokeo yake, limekuwa suala gumu sana kukutana na mtu ambaye ana nyota zote kumi na mbili. Sio tu nyota zote kumi na mbili bali hata nyota kumi na moja, kumi, tisa, nane au hata saba.
Idadi kubwa ya watu tunao waona mtaani na kudhani wamefanikiwa sana katika maisha, wanachezea kwenye nyota nne hadi tano. Hawa ni watu walio katika kundi la watu ambao katika ulimwengu wa kitabibu na kinyota wanajulikana kama watu wanao fanikiwa chini ya kiwango chao.
Wengine nyota zao hushuka hadi kuwa nusu, sifuri, hasi moja, hasi sita na chini ya hapo.
Mtu mwenye nyota sifuri ni mtu ambae katika ulimwengu wa kinyota na kitabibu anatajwa kama mtu ambae anapita duniani bila kuonekana. Ni mtu ambae riziki yake hapa duniani ni sifuri.
Mtu ambae nyota yake imeshushwa hadi kufikia hasi sita ( -6 ) ni mtu ambae katika ulimwengu wa kinyota na kitabibu tunasema nyota yake imekuwa sawa sawa na nyota ya mtu aliyelala kaburini . ( Nyota ya Kaburi / Nyota ya maiti)
Wakati mwingine nyota ya mtu inaweza kushushwa hadi kufikia hasi Arobaini na mbili ( -42). Mtu mwenye nyota hii ni mtu ambae katika ulimwengu wa kitabibu tunasema nyota yake imechukuliwa na nafsi yake imefungwa kwenye makaburi saba. Mtu alie katika kundi hili anakuwa amefungwa kwenye makaburi saba tofauti tofauti na kama ni mwanamke basi tunasema amefungishwa ndoa na makaburi saba.. Na inapotokea mwanamke akawa katika kundi hili basi mara nyingi fitna yake inakuwa imetokana na ugomvi wa kugombea mwanaume au ugomvi wa mapenzi ulio fuatia kuachana kati yake na mpenzi, mchumba au mume wake. Mwanamke huyu hukusudiwa aitulie katika ndoa yake, kila ndoa au uhusiano kwake uwe sawa na kaburi na kama kutulia basi atulie kwa mume wake wa saba ambae ni kaburi halisi.
Tofauti na mtu ambae nyota yake imeshuka na kufikia sifuri, mtu ambae nyota yake imeshushwa hadi kufikia ( -6 ) au ( -42) ni mtu ambae ramani ya maisha yake imegeuzwa juu chini ama nje ndani. Ni mtu ambae amekusudiwa kichawi kwamba, aishi maisha yake ya kaburini akiwa hapa duniani na maisha ya duniani aende kuyaishi akiwa kaburini.
Watu walio katika kundi hili ndio watu wanaokujaga kusumbua sana baadae kama mizimu mara baada ya maisha yao ya hapa duniani kufika tamati.
Sababu Kwanini Nyota Ya Mtu Inaweza Kushushwa.
Zipo sababu kuu mbili zinazo weza kufanya nyota ya mtu ikashushwa:
1. Husda, chuki na choyo dhidi ya mtu anaeonekana kuwa na nyota kubwa.
2. Ubinafsi na Tamaa ambao hupelekea mtu mmoja kuiba nyota ya mwenzake kwa ajili ya kuitumia kwa matumizi yake binafsi huku akimuacha muibiwa akiwa anahangaika ilihali alikuwa na nyota nzuri tu.
Jinsi Nyota Ya Mtu Inavyo Shushwa
Zipo njia nyingi sana zinazo weza kutumika kushusha nyota ya mtu nikisema nizitaje zote hapa ninaweza kuandika kitabu kizima. Ninacho kieleza hapa ni sababu za kitabibu zinazo weza kufanya nyota ya mtu kushuka.
Kama nilivyo sema hapo awali kuwa mwanadamu anapaswa kuwa na nyota zote kumi na mbili ili asemwe kuwa ana nyota kali. Hii ni kwa sababu mwili wa mwanadamu umegawanyika katika sehemu kumi na mbili. Kikiongezeka kitu cha kumi na tatu basi mwanadamu huyo lazima apate madhara kwa sababu anakuwa amewekwa ndani yake kitu ambacho hakina uhusiano na mwili wake.
Jinsi Inavyokuwa : Atatumwa jinni ambae nguvu yake ya kijini ni hasi ( -6 ) kwa mfano. Jinni huyu atatumwa kwenda kukaa kwenye mwili wa mwanadamu mwenye nyota kumi na mbili
Kwa sababu jinni huyu nguvu yake ama nyota yake ni ( -6 ) na anaenda kuungana na mtu ambae nguvu ya nyota yake ni 12. Maana yake ni hii ( -6 ) inajumlishwa na 12 ambapo tunapata 6. Kwa lugha nyepesi, jinni huyu atasababisha nyota ya mtu huyu ishuke kutoka 12 hadi 6 , na linapotokea jambo hilo basi mambo ya mtu huyo yanaanza kubadilika taratibu ( Majini ambao nguvu zao katika ulimwengu wa kiroho ni kuanzia ( -1 ) na kuendelea ni majini wa makaburini).
Mtu huyo huyo tena baadae anaweza kutumiwa majini wengine mfano wawili ambao kila mmoja nguvu yake ni ( -7 ). Hasi 7 mara mbili ni Hasi 14 na -14 jumlisha 6 ni Hasi 8. Mtu anapofikia hatua hii basi nyota yake inakuwa imeshushwa hadi chini ya kaburi na mambo yake yataanza kuharibika na kuwa mabaya siku hadi siku na asipo shituka mapema basi anaweza kuishia hivyo hivyo hadi umauti wake.
Njia ya pili ni ile ya kuiba nyota za mtu au watu husika. Hapa atatumwa jinni maalumu kuja kuiba nyota zote kumi na mbili za mtu Fulani na kuzipeleka kwa mchawi ambae amemtuma shughuli hiyo. Mtu ambae nyota zake zimeibiwa ataanza kuishi maisha ya mateso na kupata riziki kwake itakuwa ngumu sana kwa sababu nyota zake zinakuwa zimechukuliwa kwa nguvu na kwenda kutumia na mtu mwingine.
Mara nyingi watu w anao iba au kuagiza kuibwa kwa nyota hizi ni watu ambao hutaka kupata maradufu zaidi ya kile wanacho kitaka ambapo katika ulimwengu wa kitabibu watu hawa hulazimika kuiba nyota nzuri za watu wengine na kuzitumia kwenye shughuli zao za kutafuta riziki.
PETE YA IMMORING NA NYOTA
Pete ya Immoring ni Nini ?
Kujua pete ya Immoring Ni Nini fuatilia makala zangu za nyuma ambazo niliwahi kuandika kwa ufupi kuhusu pete hii.
Katika ulimwengu wa kitabibu na kinyota, pete ya Immoring hufanya mambo yafuatayo:
1. Pete Ya Immoring Hutumika kama Hoza la Kupooza Uchawi au Nguvu Hasi ambazo zimeelekezwa kuingia kwenye mwili wa mtu Pete ya Immoring hufanya kazi kama mmea ujulikanao kama Hoza. Mmea huu uitwao Hoza hutumika kitabibu kupooza uchawi ambao mtu ametupiwa. Hutumika kuogea, kuchanjiwa na kupikwa nyungu au kama fusho kwa lengo la kupooza uchawi ama nguvu yoyote hasi iliyo tumwa ama kujilekeza yenyewe kwenye mwili wa mtu Fulani.
Pete ya Immoring hutumika kupooza uchawi ama nguvu hasi (nguvu ya majini wabaya ) ambayo imetumwa kumuingia mtu alie ivaa. Hii hutokea pale nguvu hiyo inapokuwa kubwa kuliko nguvu ya nyota ya muhusika .
Mathalani mtu ambae nyota yake ni 12, akitumiwa jinni ambae nguvu zake ni hasi 36 jinni huyo atamdhuru mtu huyo. Sasa basi inacho kifanya pete ya Immoring ni kuupooza uchawi ama nguvu ya jinni huyo na kisha kutoa taarifa kwenye kinga ya mtu huyo kuhusu kufanyika kwa shambulio la kiroho lililo shindwa dhidi ya mtu huyo kwa lengo la kumfanya tu mhusika atambue kuwa kuna uadui umejaribu kumdhuru lakini umeshindwa.
2. Pete Ya Immoring Hutumika Kama Kinga Dhidi Ya Shari za wachawi na masheitwani wabaya
3.Hutumika kusafisha na kupandisha nyota Katika kusafisha na kupandisha nyota, aina ya pete ya Immoring itakayo tumika itategemeana na kiwango cha nyota alicho nacho mtu na kiwango cha nyota anacho kitaka. Kwa mfano mtu amabe nyota yake imeshuka hadi sifuri na anataka nyota yake ipande hadi kumi na mbili basi atalazimika kutafuta pete ya Immoring ambayo nguvu yake ni 12 . Nakadhalika.
4. Pete ya Immoring husaidia kuunganisha nyota ya mvaaji na nguvu ya mungu jua.
5. Pete ya Immoring hutumika katika matambiko yote ya jua kuanzia tambiko la biashara , kinga ya mwili, kutibu nguvu za kiume kwa kutumia tambiko la jua nakadhalika.
6. Pete ya Immoring hutumika kama mbadala wa fusho la jua. Fusho la jua ni fusho linalo tumika katika tambiko la jua.
7. Pete hii hutumika kuunganisha nguvu ya mvaaji na nguvu ya bahari.
8. Pete ya Immoring hutumika katika tambiko maalumu kwa kufanya kitu au jambo lisionekane tena kwa kutumia mawimbi tisa ya bahari na mti ulioletwa na mawimbi ya bahari au mafuriko na zaafarani nyekundu.
9.Kwa wale wanao kwenda baharini kuoga ama kuchukua maji ya bahari kwa ajili ya kutoa mikosi au kusafisha nyota basi pete ya Immoring ni nyenzo muhimu sana kwao.
10. Hutumika kuunganisha nyota ya mvaaji na nguvu ya hewa
11. Hutumika kuunganisha nyota ya mvaaji na nguvu ya ardhi
12. Hutumika kama antenna inayo fanya kazi ya kuvuta, kunasa na kuchakata nguvu zote za kiroho zinazo elekezwa kwa mvaaji
IMESIMULIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI…0744 000 473.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking