Mbunge wa (CHADEMA) Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema ameanza kupata vitisho mbalimbali kutoka kwa watu wasiojulikana wakimtishia maisha yake baada ya kusema ukweli kuhusu kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa.
Akiongea na www.eatv.tv Heche amedai kuwa ameanza kupata vitisho hivyo na kudai kuwa haviwezi kumrudisha nyuma katika kuisimamia Serikali na kuibana Serikali na kusema hawezi kubadili msimamo wake hata siku moja.
"Mtakumbuka kuwa majuzi jioni nilizungumza bungeni kuhusu kudanganywa umma juu ya mradi wa e-passports na kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa. Maelezo yangu bungeni yalitokana na Taarifa kutoka Kamati ya PAC na yalijibiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Sasa ndugu zangu nimeanza kupata vitisho dhidi ya ‘credibility’ yangu na maisha yangu. Ndugu zangu Taifa letu linapitia wakati ngumu Sana" alisema Heche
Heche aliendelea kusema kuwa
"Genge la wahalifu wa ki Uchumi na kisiasa kamwe lisitarajie nitatishika ama kubadili msimamo. Vitisho vilivyoanza dhidi yangu baada ya kuibua Ufisadi Katika Vitambulisho vya Taifa na E -Pasport havitaniogopesha kamwe. Njia zao ovu ama kunitisha ama kutaka kuchafua heshima yangu ama kunitengenezea kesi ama kuninifanyia alichofanyiwa Mhe. Tundu Lisu hazitanirudisha nyuma" alisisitiza Heche
Mbali na hilo Heche ameweka wazi kuwa kwa sasa anaandaa nyaraka muhimu ili azipeleke Bungeni kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika Vitambulisho vya Taifa pamoja na E- Passports.
Source:to muungwana blog
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking