Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Jana February 2/ 2018 alifanya ziara ya kutembelea na Kukagua Ujenzi wa majengo mapya ya Maabara, Jengo la mama na mtoto, Jengo la upasuaji Pamoja na Ujenzi wa Nyumba ya mganga katika kituo cha Afya Mlangali Kituo ambacho kimepokea Jumla ya Tsh, Million 500 Kutoka Serikali kuu kwaajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Kituo hicho cha Afya.
Katika Ziara yake katika Kata ya Mlangali Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olle Sendeka Aliambatana na Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe bw, Hosea Mpagike, Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe pamoja na Wataalamu wa idara mbalimbali za Mkoa Huo.
Akiwa katika Kituo cha Afya Mlangali kukagua maendeleo ya Ujenzi huo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Sendeka aliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Katika kukagua majengo hayo ambayo yameshaanza kujengwa na yamefikia Katika Hatua ya Msingi ambapo Ujenzi unaendelea Katika Hali ya kuridhisha kwakutumia Nguvu za wananchi.
Awali Kabla ya Kupokea kiasi cha Tsh, Milioni 500 Kutoka Serikali kuu Kituo hicho cha Afya Mlangali kilipokea kiasi cha Tsh, Milioni 59 Kwaajili ya Ujenzi wa Jengo la upasuaji na Wodi ya kupumzikia wagonjwa ambapo Katika matumizi ya pesa hiyo Mh, Mkuu wa Mkoa wa Njombe alisema kuwa Licha ya kuwa umepita muda mrefu lakini majengo hayo hayajakamilika hivyo atahakikisha kuwa Mkandarasi aliyekabidhiwa Kazi hiyo anapatikana pamoja na Wataalamu waliosababisha Majengo hayo kutokamilika wanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheri.
Akihutubia Mamia ya wakazi wa kata ya Mlangali waliojitokeza kumsikiliza Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe Katika Viwanja vya MTC Mlangali Mh, Sendeka Aliwapongeza Wakazi wa kata ya Mlangali kwa Moyo wao wakujituma Katika Shughuli za Ujenzi wa kituo cha Afya na kuwataka wananchi hao kuendelea kujitolea ili kazi hiyo ikamilike mapema kwakuwa wameshapata Pesa ya kutosha kutoka serikalini Kiasi cha Tsh. Million 500.
Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Mlangali Kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh, Hamis Kayombo Alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwakuwatembelea wananchi wa Kata ya Mlangali huku akimuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe kuwa Shughuli za ujenzi wa kituo hicho cha afya zitakamilika kwa muda muafaka kutokana na Ushirikiano mzuri uliopo Kati ya Viongozi na Wananchi wa kata ya Mlangali.
Katika hatua nyingine Madereva wa pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Katika Stendi ya Mlangali waliwasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe wakidai kuwa Askari wa usalama Barabarani Mlangali wamekuwa wakiwakamata mara kwa Mara wawapo barabarani na kuwapiga Faini kubwa kiasi cha Tsh, 30,000 kwakosa moja bila hata kukatiwa Risiti Jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Sendeka aliamua kutoa wito kwa Askari wa usalama barabarani Wilaya ya Ludewa kufanya Kazi kwa ushirikiano Na Bodaboda hao kwakuwa nao ni wadau wa Jeshi la polis na Serikali kwaujumla.
Mh, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Pia Amepiga marufuku Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwatoza Ushuru wafanyabiashara wadogo wa Mkaa ambao awali halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilikuwa ikiwatoza ushuru wauzaji hao wa Mkaa zaidi ya Tsh, 300,000 kwaajili ya Leseni ya kufanyia Biashara hiyo ya Mkaa na Kumuagiza mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere kusimamia maagizo hayo ya mkuu wa Mkoa.
"Mtu alipanda miti yeye mwenyewe kwa gharama zake na wakati anapanda hakuna hata mtumishi wa serikali aliyemsaidia anauza mkaa wake Debe moja au mbili rejareja huko vijijini halafu uje umwambie alipe kibali 300,000, Kwa Mkoa wangu wa Njombe nasema Hapana labda wale wanaosafirisha kwa magari makubwa hao ndio walipe maana hao wanamtaji Mkubwa Namwambia aliyewaambia mlipe hiyo pesa iwe mwisho na Uzeni Sana Hakuna mtu atakae wagusa, Narudia Uzeni Sana Hakuna Mtu atakaye wagusa "
Nikauli ya Christopher Olle Sendeka Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Akishiriki ujenzi wa Msingi wa majengo ya Kituo cha Afya Mlangali katika picha Mkuu huyo wa wilaya Akiwa na Mwiko wa ujenzi na Jiwe mkononi.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking