NAIBU
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia,William OleNasha,amefafanua
utaratibu wa kupata cheti mbadala/uthibitisho kwa mtu aliyepoteza cheti
ambapo ameeleza kuwa Baraza la Mitihani litafanya kazi hiyo kwa muda
usiozidi siku 30.
Ole
Nasha aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Mafinga Mjini,Cosato Chumi (CCM) lililokuwa likihoji ‘’Je
ni utaratibu gani unaotumika pale mtu anapopoteza cheti ili aweze kupata
cheti kingine’’?,Je ni unapata cheti halisi au nakala? na ni taratibu
gani anatakiwa kuzifuata mtu ili ombi lake lifanyiwe kazi ipasavyo na
bila kucheleweshwa?.
Katika
majibu yake Naibu Waziri huyo alieleza kuwa mhitimu aliyepoteza cheti
hupatiwa cheti mbadala/uthibitisho wa matokeo kwa kutoa taarifa kwa
Jeshi la Polisi kuhusu upotevu wa cheti na kupata hati ya upotevu.
Pia
mtu aliyepotelewa na cheti atatakiwa kutangaza gazetini kuhusu upotevu
huo kwa lengo la kuutaarifu umma ili kusaidia kukipata na endapo cheti
hakitapatikana hata baada ya kufuata utaratibu huo ,mhitimu atajaza fomu
ya ombi la cheti mbadala /uthibitisho wa matokeo na kuiwakilisha Baraza
la Mitihani.
‘’Baada
ya mhitimu kujaza fomu hiyo Baraza la Mitihani hufanya uchunguzi wa
uhalali wa umiliki wa cheti husika na kutoa huduma stahiki ,wahitimu
waliofanya mtihani kuanzia Mwaka 2008 ambao vyeti vyao vina picha
hupatiwa vyeti mbadala ‘’alisema na kuongeza kuwa
“Na
waliofanya mtihani kabla ya Mwaka 2008 hupatiwa uthibitisho wa matokeo
ambao hutumwa kwa waajiri wao au mahali pengine kwa mahitaji
yaliyotolewa na mwombaji na kundi hilo halipewi cheti mbadala’’
Alisema
cheti mbadala kinachotolewa ni cheti halisi ambacho huongezwa maandishi
yanayosomeka ’DUBLICATE’ kuonyesha kuwa cheti hicho kimetolewa mara ya
pili.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking