Na Judith Mhina – MAELEZO
Agizo
la Rais John Pombe Magufuli la kuipatia Kampuni ya Said Salim Bakhresa
(SSB) Group LTD ardhi yenye ukubwa wa ekari 10,000 kwa ajili ya kuwekeza
katika kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari katika Wilaya ya
Bagamoyo, mkoani Pwani limetekelezwa.
Msemaji
wa Makampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD, Bw Hussein Sufian
ameiambia Idara ya Habari (MAELEZO) katika mahojiano maalumu ilipokuwa
ikifuatilia utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilolitoa tarehe 6
Oktoba, 2017 baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Kampuni
hiyo kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.
Bw.
Sufian amesema, tayari Kampuni yake imetenga takriban Shilingi Milioni
75/- kwa ajili ya kuanza uwekezaji katika shamba hilo kwa shughuli za
kilimo cha miwa na kufafanua kuwa, hatua ya awali ya upandaji wa miwa
kwenye vitalu imeanza.
Amesema,
maandalizi ya upandaji wa miwa katika Kitalu A chenye ekari 48
umekamilika. Aidha, upandaji wa miwa katika eneo la jumla ya ekari 8
kati ya hizo utaanza tarehe 3 Februali na ekari nyingine 40 utafanyika
mwezi Juni na Julai, 2018.
“Baada
ya kukamilika kwa upandaji katika Kitalu “A” mwaka huu (2018),
tunatarajia ifikapo Januari na Juni 2019 tutaendelea kupanda miwa kwenye
kitalu “B” chenye ukubwa wa ekari 300. Mzunguko huo utaendelea hivyo
hivyo mpaka kufikia hekari 2030 ambazo tumekusudia kuanza ujenzi wa
kiwanda mapema 2019 na uzalishaji wa sukari kiwandani ifikapo Septemba
2020,” alisema Sufian.
Akielelezea
zaidi juu ya mradi huo, Bw. Sufian amesema kwamba tayari watu 50
wameajiriwa, kati ya hao 20 ni wa kudumu na 30 vibarua. Watu 5 wanafanya
kazi za kiufundi na 45 nguvu kazi. Aidha, Kampuni hiyo imeajiri
Wataalamu 2 kutoka nje ambao ni Bw. Abraham Star Mtaalamu wa Umwagiliaji
kutoka Israel na Mtaalamu wa Kilimo cha miwa kutoka India, Bw Narayan
Krishna, kiwanda kinakusudia kuajiri watu 1000 ifikapo mwaka 2020.
Ili
kilimo hicho cha miwa kiwe endelevu, pamoja na mambo mengine uchimabji
wa visima na utengeneaji wa mabwawa matatu umefanyika ambapo maji
yanavutwa kutoka mto Wami kilometa 5 mpaka katika bwawa lililotengenezwa
la Tambezi 1.
Maji
yanapojaa yanavutwa kupelekwa bwawa dogo katika Kitalu A na sehemu ya
mitambo ya kuchuja maji, ambapo kila Kitalu kitakuwa na kituo cha
kusukuma maji na kupeleka kwenye mabomba makubwa kisha madogo yanayopita
katikati ya mimea iliyopandwa na kufanya umwagiliaji wa matone.
Agizo
la Rais Magufuli lilikusudia kuondoa pengo la uzalishaji wa sukari kwa
matumizi ya kawaida nchini ambapo katika kipindi cha mwaka 2016/ 2017
mahitaji yalikawa ni tani 590,000 kati ya hizo tani 135,000 ni mahitaji
ya kiwandani na 455,000 ni mahitaji ya kawaida ya binadamu.
Uzalishaji
wa sukari nchini ulikuwa tani 350,846 na kufanya kuwa na upungufu wa
tani 259,156. Hivyo uzalishaji wa tani elfu 30 mpaka 70 utaondoa pengo
la uhaba wa sukari nchini Tanzania.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking