Dinsdag, Februarie 06, 2018

Serikali kutunga sheria ya kilimo ambayo itatoa mwongozo kwa wadau wa sekta ya kilim


Waziri wa kilimo Mh.Dkt.Charles Tizeba amesema serikali inakusudia kutunga sheria ya kilimo ambayo itatoa mwongozo na kanuni za kufuatwa na wadau wote wa sekta ya kilimo nchini ili kuongeza uwajibikaji zaidi na kuinua kilimo kwa shabaha ya kuondokana na kilimo cha mazoea
.

Akizungumza wakati wa ziara ya kujionea utekelezaji wa kilimo cha Pamba katika wilaya ya kwimba mkoani Mwanza,Mh.Dkt.Tizeba amesema sheria hiyo itasaidia katika kuhakikisha wadau wote wa kilimo wanashiriki ipasavyo katika kumsaidia mkulima kulima kwa tija na kitaalam ambapo yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo atawajibishwa.

Waziri Tizeba pia amekerwa na tabia ya maafisa kilimo kukaa ofisini na kushindwa kwenda kusimamia kilimo cha zao la pamba hivyo kusababisha wadudu aina ya funza na utitiri kuendelea kushambulia zao hilo kutokana na wakulima kukosa elimu ya kanuni 10 za kilimo bora.

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Simion Msafiri akizungumza na watumishi wa ya idara ya kilimo na ushirika wilayani humo amelalamikia kuwepo kwa viuadudu vya zao la pamba ambavyo muda wake wa matumizi umekwisha tangu mwaka 2016 na kuagiza wakulima wairudishe hata kama ni makopo ili isiendelee kutumika msimu huu.

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya pamba nchini Marco Mutunga amesema zaidi ya chupa laki mbili na elfu hamsini za viuadudu tayari zimepokelewa kwenye ghala la bodi ya pamba lililopo igogo jijini Mwanza na zitaanza kusambazwa kwa wakulima wote kuanzia Februri sita siku ya Jumanne ili kuhakikisha kila mkulima anapulizia dawa hiyo kwa ajili ya kuangamiza wadudu aina ya funza na utitiri.
Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking