Woensdag, Februarie 07, 2018

USHIRIKINA WAINGIA SHULENI LUDEWA, WATOTO WAPELEKWA SHAMBANI



Mwandishi wetu Ludewa

Tatizo la kuanguka mara kwa mara kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muholo iliyopo katika Kijiji cha Muholo kata ya Luana Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Iimeilazimu kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Ludewa Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ambae ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Kufika katika Kijiji Hicho ili Kubaini Tatizo.

Mapema Siku ya Jana February 06 / 2018 Baada ya Kufika katika Kijiji cha Muholo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere aliwataka Wananchi wa Kijiji cha Muholo Kueleza Sababu inayowafanya watoto waanguke wakiwa Shuleni Ambapo Wananchi hao wa kijiji cha Muholo walimweleza Mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa kuwa Tukio hilo lilianza Tangu 27 October 2017.

Wananchi hao ambao ni Wazazi wa wanafunzi wanaoanguka katika Shule ya Msingi Muholo waliendelea kumweleza Mkuu wa wilaya ya Ludewa kuwa Baada ya Kuanguka watoto hao wamekuwa wakilia na kutaja Majina ya baadhi ya Wakazi wa Muholo wakisema kuwa wanapigwa Makofi Usoni na Fimbo Huku wakitaja Majina ya Bw,Wadhiki, Athumani pamoja na Mdanga Kuwa wanawatumikisha kishirikina Kufanya Kazi zao za Kulima Shambani, Kubeba Mbao huku wakilishwa chakula cha Pumba na Nyama za Binadamu waliooza.

Aidha watoto hao Wakiulizwa na wazazi wao wakiwa katika hali ya kupoteza Fahamu wamekuwa wakieleza kuwa Wanasafirishwa na watu hao waliotajwa kisha kupelekwa katika mashamba yao kufanya kazi wengine wamekuwa wakipelekwa Manda huko ziwa nyasa kucheza Mpira na wawapo Shambani Wasipofanya kazi Wanachapwa Viboko huku miili yao ikiwa inavimba na Baada ya Kupata fahamu watoto hao hukataa kabisa kueleza yanayowasibu.

Wananchi wa Kijiji Cha Muholo walisema kuwa Baadhi ya waliotajwa kama wahusika wa Tukio hilo akiwemo Bw, Athumani wamekuwa wakifanya Matukio hayo kutokana na kwamba Serikali ilijenga Shule hiyo katika Eneo la muhusika huyo ambae hajaridhika kulitoa Eneo hilo.

Kwaupande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Muholo Bw, George HauleAlithibitisha kutokea kwa Tukio hilo na kusema kuwa Baada ya kupoteza Fahamu kwa watoto hao Uongozi wa Shule umekuwa Ukiwashirikisha Wataalamu wa Afya na Wachungaji ambao maranyingi wamekuwa wakiwaombea watoto hao na maombi yao yameonekana Kuzaa matunda.

Baadhi ya watuhumiwa Wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Ludewa Mjini kwakuwa walikiri Mbele ya wananchi wenzao kuwa Ndio wahusika wa tukio hilo huku wakisema kuwa Hawatarudia tena kufanya Matukio hayo ya Uhalifu wa Kishirikina ambapo kwa maagizo ya Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Watuhumiwa hao wanatakiwa Kukiri kwa Maandishi katika kituo cha Polisi ili Tatizo hilo lisijirudie na Hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking