Wafanyakazi wa kiwanda cha chai cha kibena wilayani Njombe Mjini katika Mkoa wa Njombe wanaulalamikia Uongozi wa Kiwanda hicho kwa madai hawatendewi haki stahiki zinazo takiwa kutendewa kwa mujibu wa sheria za kazi.
Hali kadhalika wafanyakazi hao wamezidi kuongea na vyombo vya habari kwa jinsi wanavyo tumikishwa kwenye kiwanda hicho ni pamoja na kujaziwa mikataba ya muda mfupi pamoja na kuto kulipwa mishahara yao kwa wakati mwafaka na wakaongeza kwa kusema kuwa kiwanda hicho cha chai kimeleta wawekezaji wengine na wao kama watumishi wa kiwanda hicho hawajatambulishwa.
Sambamba na hilo wafanyakazi hao wamesema kuwa uwepo wa kiwanda hicho mkoani hapo kilikuwa na msaada mkubwa kwenye maisha yao lakini sasa kimekuwa ni kiwanda ambacho kinawatesa wafanyakazi moja ya wafanya kazi hao ambaye alijazishwa mkataba wa mda mfupi alipo kuwa katika majukumu yake ya kazi aliumia kwa majeraha na baada ya kutoka hospitali alifukuzwa kazi bila kulipwa mahitataji yake stahiki.
Hata hivyo wafanyakazi hao walizidi kusema kuwa unyanyasaji wanao upata kwenye kiwanda hicho ni mkubwa na wameongeza kwa kusema kuwa wanafanyishwa kazi hadi saa sita usiku bado asubuhi na mapema wanatakiwa kuludi kazini tena.
Bado wafanyakazi hao hawakuishia hapo walizidi kuwaeleza waandishi wa habari kuwa wao wanajiona tayari wamesha uzwa kwa watu wasio julikana na wakaweka bayana kuwa taarifa ya manyanyasiko hayo waliwaomba viongozi wa tipau kumfikishia taarifa mkuu wa mkoa huo na hawajaona kinacho endelea.
Mwanamke mmoja akawaeleza waandishi wa habari kuwa waajiri wa kiwanda hicho wamekuwa na tabia ya kuwatengenezea rushwa watu wanao hitaji kazi.
Pia jitihada za kumtafuta msemaji wa kiwanda hicho ambaye ni meneja mwajiri anaye fahamika kwa majina ya MUHAMEDI KIBAO alikataa kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai yeye amekahimu kazi hiyo na hawezi kuzungumza siku ya leo alisema kuwa yupo anaye stahiri kuzungumzia Swala hilo.
Waandishi wa habari hawakuishia hapo wakamtafuta kwa njia ya simu kiongozi wa kiwanda hicho anaye fahamika kwa majina ya Valeliani Aseyi ambaye ni msimamizi wa viwanda zaidi ya vitatu ambavyo ni Ikanga,Luponde,Kibena na Itona alijibu kuwa yeye hawezi kuzungumza kwa njia ya simu mbaka aandikiwe barua itakayo weza kumfanya ajibu hilo kwa waandishi wa habari.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking