Wafanyakazi
wa umma nchini Burundi wameanza kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao
kwaajili ya kufadhili uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2020.
Katika
kipindi cha miaka miwili ijayo, raia wote wa Burundi walio na zaidi ya
umri wa kupiga kura wa miaka kumi na minane na zaidi, ni sharti
wachangie katika hazina hiyo ya kitaifa.
Serikali
ya Burundi imesema imechukua uamuzi huo ili kuziba pengo
lililosababishwa na uamuzi wa wafadhili wa kuzuia misaada tangu mzozo wa
mwaka 2015 wakati rais Pierre Nkurunziza alipowania muhula wa tatu.
Hata
hivyo serikali imekariri kuwa hazina hiyo ya uchaguzi ni wazo la raia
wa Burundi wenyewe, pendekezo ambalo limepingwa na wakuu wa vyama vya
wafanyakazi.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking