Na Tiganya Vincent-rs Tabora
Vitambulisho
wa uraia vitasaidia kuwa na utambuzi wa wananchi utakao ondoa ile tabia
ya baadhi ya watu kutilia mashaka wakati wa shughuli mbalimbali ikiwemo
kipindi kushiriki katika zoezi la uchaguzi wote wote.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dkt.Mwigulu Nchemba wakati uzinduzi wa zoezi la usajili wananchi kwa
ajili ya vitambulisho vya kitaifa mkoani humo.
Alisema
kuwa mara nyingi mtu anapogombea nafasi yoyote hapa nchini au
kunapokuwepo na migogoro ya kugombania mashamba ndio suala la kusema
kuwa huyo sio raia linapojitokeza.
Dkt.
Nchemba alisema wananchi wenye sifa kuchangamkia zoezi la usajili na
upataji wa vitambulisho vya uraia ili kuepuka matatizo kama vile
migogoro ikiwemo ya mapingamizi wakati chaguzi mbalimbali na kuiweza
Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya wananchi
wake
Alisema
kuwa hata uchumi wa kisasa unaanza na kutambua kwa Serikali kutambua
watu iliyonao na ndipo ipange mipango ya maendeleo kwa ajili yao.Waziri
huyo aliongeza kuwa hata kwenye vyombo vya fedha kama vile Benki
zimekuwa zikiweka riba kubwa katika mikopo kwa sababu ya baadhi wananchi
kukosa utambulizi
Naye
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Andrew Massawe alisema jitihada hizi zote zimelenga kusaidia Serikali na
wananchi kutambulika na hatimaye Mashirika, Taasisi na Makampuni nchini
kutumia mfumo huu kutoa huduma zenye ubora na tija kwa Taifa.
Alisema
mfumo huu una faida nyingi kwa Taifa na mwananchi mmoja mmoja kama vile
kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi, wananchi kutambulika kwa haraka
pindi wanapofika kupata huduma za afya na Elimu.
Massawe
alisema kuwa faida nyingine ni kurahisisha utambuzi wa makundi yenye
mahitaji maalumu ikiwemo utambuzi wa kaya masikini unaofanywa na Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na upatikanaji wa huduma za kifedha na
Simu kirahisi.
Kwa
upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi aliwaagiza viongozi
wa ngazi zote mkoani humo kuhakikisha kuwa anayesajiliwa na kupata
kitambulisho cha uraia ni yule mwenye sifa na sio mgeni.
Alisema
Serikali ya Mkoa wa Tabora haitasita kumchukulua mtu yoyote
atayeshiriki katika udanganyifu utaosababu watu wasio raia kupata
vitambulisho vya uraia.
Queen
alisema kuwa kila mmoja ni vema akasimama katika nafasi yake
kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu
ili kuleta ufanisi.
Alitoa wito kwa jamii kusaidia kuwafichua watu wasio raia wanaotaka kujipenya ili wapate vitambulisho vya uraia
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking