Na mwandishi wetu
Ludewa
Huyu ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Mmanda Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe
Prisca Jonathani Mwakakae.
Prisca Jonathani Mwakakae.
Wananchi wa kijiji cha Manga katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
wameandamana leo jully 6.2018
katika
ofisi za kijiji hicho wakifunga milanga ipatayo saba ya ofisi hizo kwa lengo la
kutaka viongozi wa juu waende kutatua mgogolo wa aridhi ambayo inapiganiwa na
Bwana Frorence Mtewele kuwa ni mali yake
na huku viongozi wa kijiji hicho wakidhibitisha kuwa ni eneo la serikali.
Katika hatua nyingine
wananchi hao wamesema eneo hilo tangu zamani lilikuwa likimilikiwa na serikali
ya kijiji hicho tu baada ya kupewa na mzazi wa bwana frorence mtewele ambapo
kwa sasa kijiji hicho kimewekeza kwa zao miti.
Hali kadhalika Mwenyekiti
wa kijiji hicho ndugu Angerusi Mgaya amezungumza na waandishi wa habari kwa
kudhibitisha kuandamana kwa wananchi hao na akaongeza kwa kusema kuwa mgogoro
wa eneo hili sio wa mara ya kwanza kwa kusema kuwa hata mkuu wa wilaya ya
ludewa alishawahi kufika katika eneo hilo na kumaliza kuwa eneo hilo ni la
serikali.
Akaongeza kwa kusema
kuwa yeye kama mwenyekiti wa kijiji hicho amejalibu kuzungumza na viongozi wa
kata hiyo na viongozi hao bado hawaja mpa majibu yoyote juu ya mgogoro huo.
Sambamba na hilo Afisa Mtendaji
wa kijiji hicho ndugu Prisca Jonathani Mwakakae
amesema kuwa wananchi kuandamana katika eneo hilo wapo sahihi kwa kudai mali ya
kijiji chao na akaongeza kwa kusema kuwa licha ya maandamano salama yeye kama
kiongozi wa kijiji hicho ameamua kutoa taarifa kituo cha polisi wailaya ya ludewa na kwa viongozi
wake wa juu.
Hata hivyo ndugu Frorence
Mtewele ambaye ndiye mmiliki wa eneo hilo amesema kuwa yeye eneo hilo linalo
gombaniwa ni mali ya babayake tangu hapo zamani
Pia akamaliza kwa
kusema kuwa kindi kilicho pita wiki kdhaa nyuma alipaelekwa mahakamani juu ya
eneo hilo na mahakama ikaamuru kuwa eneo hilo ni la kwake na mahakama ikaamuru
kuwa ambaye hajalika na kesi hiyo anaruhusiwa kukata rufaa.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking