Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba
jana usiku amefanya ziara ya kushtukiza katika maduka makubwa ya kuuza
sukari na mchele jijini Dar es salaam,na kubaini kuna uingizwaji wa
bidhaa hiyo kimagendo na kutoa agizo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata
wahusika.
Kwa
sasa wafanyabiashara hao wametiwa nguvuni na suala hilo limefikishwa
Polisi kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine za kisheria pindi
uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa hao watapandishwa kizimbani
Waziri
wa Kilimo akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari
Tanzania Miraji Kipande amesema kuwa uuzwaji wa bidhaa hizo unahitaji
mfanyabishara kufuata na kukamilisha utaratibu , hivyo wafanyabiashara
wanaouza sukari na mchele kinyume cha sheria, Kanuni na taratibu za nchi
wawajibishwe mara moja.
Katika
ziara hiyo Waziri amekuta Sukari na mchele uliokuwa ukiuzwa na
wafanyabiashara hao kinyume na taratibu za nchi, Sukari iliyokutwa
ilikuwa imefungashwa katika ujazo wa kilo moja moja na zilisomeka kuwa
zimetoka nchini Mauritius na Uingereza ambazo ziliingizwa nchini bila ya
kuwa na kibali cha Waziri Mkuu au Bodi ya Sukari Tanzania ambayo ipo
chini ya Wizara ya Kilimo.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking