Na. Chrispin Kalinga - Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe.
Anthony Mtaka tarehe
11 Januari 2024 aliongoza Mkutano wa Pareto na Mdau Mkuu wa PCT
uliofanyika katika Ukumbi wa Madihani Villa Hotel ulipo Halmashauri ya Wilaya
ya Makete.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya hiyo, Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Kilimo kutoka
Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe pamoja na Wananchi wa maeneo hayo
wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda.
Alipokuwa akizungumza na wananchi
waliojitokeza kwenye
mkutano huo Mhe. Mtaka alisema kuwa, Wilaya ya Makete inakwenda kukua
kiuchumi kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa haswa kwenye maeneo ya Kilimo
cha Pareto pamoja na Kilimo cha Ngano.
Aidha, Mhe. Mtaka alisema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete yenye kata 23, jumla
ya kata 21 zinafaa kwa Kilimo cha zao la Pareto ambapo jumla ya eneo lenye
ukubwa wa Hekta 2800 zinafaa kwa Kilimo cha zao la Pareto katika kata 21.
Ikumbukwe kwamba zao la Pareto
hapa nchini Tanzania linaumuhimu mkubwa kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja
na utengenezaji wa madawa mbalimbali ya kuua wadudu ambapo makampuni ya madawa
duniani hutumia sumu ya Pareto katika kutengeneza madawa (Viuadudu), Unga wa
maua ya Pareto hutumika kuhifadhi nafaka kama vile mahindi, Maharage ili
yasishambuliwe na wadudu waharibifu.
Sambamba na hayo Mhe.
Mtaka alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuutazama na kuukuza
kiuchumi Mkoa wa Njombe kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya
kilimo ambapo amesema, Wilaya ya Makete ina jumla ya Maafisa Ugani Kilimo 59,
ambapo kati ya hao watatu (3) wapo ngazi ya Makao Makuu ya Wilaya hiyo na
Maafisa Ugani 56 wapo ngazi ya Kijiji na Kata na wote hao wamepatiwa Pikipiki
kwaajili ya Utendaji kazi wa kuwahudumia wakulima.
Uwepo wa Maafisa Ugani ngazi
hizo unasaidia kutoa ushauri wa Kitaalam kwa wakulima ngazi ya Jamii, Watendaji
wa Kata na Vijiji wanasaidia katika uhamasishaji wa Kilimo cha Pareto na
Kuwezesha tija na uzalishaji kuongezeka.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking