Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.
Anthony Mtaka amewataka wanafunzi na wananchi wa mkoa wa Njombe kwa ujumla
kubadili namna ya ulaji wa vyakula ili kuepukana na changamoto mbalimbali
zinazotokana na ulaji mbaya, na ameshauri umuhimu wa kuzingatia lishe bora huku
akisisitiza kwamba lishe bora ni kupata mlo kamili na sio kushiba kama
ilivyozoeleka kwa jamii nyingi ikiwepo wanafunzi ambao baadaye ndio Taifa la
Kesho.
Hayo aliyasema tarehe 17Januari 2024 alipofanya ziara
katika shule ya Msingi Nazaleti iliyopo Halmashauri ya Mji Njombe alipokuwa
akitoa elimu ya Lishe ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni yenye lengo la kutoa elimu ya lishe kwa wazazi na
walezi na namna bora ya ulaji unaozingatia afya.
‘’Lishe bora inaanza na namna ya
ulaji kwani lishe bora sio kula na kushiba hivyo ninyi kama taifa
la kesho mnapaswa kuzingatia namna ya ulaji bora kutokana na changamoto
mbalimbali za kiafya zinazotokana na ulaji mbaya kwani kumekuwa na wazazi
wenye tabia ya kupika vyakula leo chakula hicho kikaliwa na watoto wiki nzima
sasa ninyi watoto leo tumewapa elimu hii ya lishe mkawe mabalozi kwa
wazazi.amesema Mtaka
Mhe. Anthony Mtaka aliongeza kuwa, watoto wanapaswa kula kwa
kuzingatia afya jambo ambalo litasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za
kiafya ikiwa ni pamoja na Ukondefu na Udumavu kwa kutumia vyakula vinavyolinda
mwili na kuwataka kuacha mara moja kula vyakula ambavyo vitawasababishia
madhara ya kiafya kwa baadaye.
Kampeni ya Lishe Mkoa wa Njombe
inaendelea ikiongozwa na Kauli mbiu isemayo, "Lishe ya Mwanao ni
Mafanikio yake Njombe tunaweza". Kujaza tumbo si lishe jali unachomlisha.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking