Njombe
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya sera, Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama
Tarehe 14 Januari 2024 alikuwa mgeni
rasmi wakati wa kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Dkt. Eusebius Kyando Askofu wa
Jimbo la Njombe akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati akitoa salamu za serikali
Mhe. Jenista Mhagama aliwaomba
viogozi wa dini nchini kuendelea kulinda Amani na
Mshikamano wa Taifa letu.
Mhe.Mhagama alisema kuwa, tunu hizo ndizo zinazolitambulisha Taifa
letu la Tanzania duniani na ulimwenguni kote.
"Tunu hizi zilindwe kwa
kuzingatia umuhimu wake, pia Serikali inawashukuru viongozi wote wa dini
kwakuendelea kuliombea Taifa, tunaomba muendelee kuliombea taifa bila
kuchoka" alisema Mhe. Waziri
Mheshimiwa Waziri alipokelewa na
kukaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka, wakati
akimkaribisha kiongozi huyo Mhe. Mtaka aliwaomba viongozi wa dini
kwakushirikiana na serikali kwa pamoja kuunga mkono jitihada zinazofanywa
kwenye sekta ya elimu hasa katika masuala ya Lishe kwa wanafunzi mashuleni kwa
lengo la kutokomeza udumavu na utapiamlo.
Viongozi mbalimbali wa serikali
na viongozi wa Vyama vya kisiasa walihudhulia
shughuli hiyo muhimu iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking