Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh.Christopher Ole Sendeka amemvua cheo cha ukuu wa shule na kumtaka ahamishwe katika shule hiyo mara moja mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Manda Oraph Mwinuka wilayani Ludewa kutokana na mwalimu huyo kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa madarasa, Daharia pamoja na kushuka kwa ufaulu katika shule hiyo.
Hayo yalifanyika February 3 katika ziara ya mkuu wa mkoa,ziara ambayo ilifanyika katika wilaya ya Ludewa ikiwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maendeo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Vituo vya Afya,Shule na Maji,miradi ambayo imepata fedha kutoka Serikalini.
Mh.Sendeka alimtaka mwalimu mkuu huyo kukabidhi ofisi kwa makamu wake kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa katika shule hiyo ikiwa Serikali imetoa Zaidi ya shilingi milioni mianne tangu mwaka 2016 lakini mpaka leo miradi hiyo imekuwa ikisuasua ili hali fedha ipo.
Katika ziara hiyo Mh.Sendeka alitembelea ujenzi wa majengo mapya ya kituo cha afya cha kata ya Mlangali ambapo Serikali imepeleka jumla ya shilingi milioni miatano,mradi wa maji kata ya Ludewa mjini wenye thamani ya shilingi milioni mianne,ujenzi wa Dahalia,madarasa na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Manda wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni mianne.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa jengo la upasuaji na majengo mapya ya kituo cha afya cha kata ya Manda yanayoghalimu kiasi cha shilingi milioni mianne,fedha hizo zote zimetolewa na Serikali lakini wananchi wanatakiwa kuchangia nguvu zao ili miradi hiyo ikamilike kwa haraka.
“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Serikali yake ametoa fedha za maendeleo ili wananchi waweze kupunguziwa mzigo wa kuchangia katika ujenzi lakini inashangaza kuona baadhi ya watendaji wa Serikali wanakwamisha mipango ya Serikali hivyo sitawavumilia watakaojaribu kufanya hivyo”,alisema Mh.Sendeka.
Mh.Sendeka pia alifafanua kuhusiana na mpango wa chakula shuleni kuwa wenye jukumu la kukusanya chakula na michango yake ni wazazi wenyewe na sio walimu hivyo kauli ya Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya elimu bure na kuzuia michango mashuleni ilikuwa na lengo la kuwapatia nafasi walimu kubaki katika ufundishaji.
Aidha aliutaka uongozi wa wilaya ya Ludewa kuwasimamia ipasavyo wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali wilayani hapa ili iweze kuendana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mwisho.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking