Na Nimrod Mgoye.
Wananchi mkoani Njombe wameiomba serikali kuongeza nguvu ya usimamizi kwa wakandarasi wa miundombinu hususani ya barabara zinazojengwa mkoani NJOMBE yenye thamani ya Zaidi ya bilioni 400 ili kuwezesha miradi hiyo kujengwa kwa kiwango na kukamilika kwa wakati.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi wa kata ya Njombe mjini wanasema awali kabla ya kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara hususani kipande cha Lusitu-Mawengi kuelekea wilayani Ludewa inayojengwa kwa kiwango cha Zege wanasema awali hali ya usafiri ilikuwa ni ngumu huku gharama za usafirishaji zikiwa juu.
Kwa upande wake katibu wa itikadi siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe ndug. Erasto ngole wakati akizungumza na waandishi wa habari anasema serikali ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na TANROD wanasimamia vema ujenzi wa miundo mbinu hiyo huku akiongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara nne kubwa zitawaunganisha wananjombe na fursa mbali mbali za maendeleo.
Naye mkuu wa mkoa wa Njombe mh.CHRISTOPHER OLESENDEKA anasema serikali ya mkoa wa Njombe itaendelea kusimamia kikamilifu na kukamilisha kwa wakati miradi yake ikiwemo nyumba za serikali.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking