Vrydag, September 07, 2018

Uhamiaji: Wachungaji Acheni Kualika Wahubiri Kutoka Nje Ya Nchi


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Afisa uhamiaji katika jijini la Dodoma Edwin Mwasota amewataka wachungaji na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya Kikristo mkoani Dodoma kuacha tabia ya kualika wachungaji kutoka nje ya Tanzania na kufanya mahubiri katika jiji hilo bila kibali Maalum.
 
Bwana Edwin ameyasema hayo  Septemba 5 katika moja ya Ziara ya mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobass Katambi kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata za Ipagala na Mnadani jijini Dodoma.
 
Afisa Uhamiaji huyo amesema kuwa wahubiri wazawa wana uwezo wa kuhubiri hivyo kufanya mialiko ya kualika wahubiri kutoka nje ni kujidhihisha kuwa wao hawawezi na kubainisha kuwa katika jiji la Dodoma pamekuwepo na wimbi la mabango ya matangazo ya wahubiri kutoka nje ya Tanzania ikiwemo Kenya bila Uhamiaji kujulishwa juu ya ugeni huo.

"Hivi nyie wachungaji hamjiamini  kuhubiri?sasa kumeibuka wimbi la wahubiri kutoka nje ya nchi.Ukifuatilia mtu huyo kaingiaje hapa jijini Dodoma hauwezi kuelewa mwanzo wala mwisho.Ukienda kila mtaa  hususan kwenye nguzo za TANESCO utakuta kuna mabango ya matangazo  ya Ujio wa
wahubiri kutoka nje ya nchi mfano Kenya,Uganda.Sasa unajiuliza huko anakotoka hakuna watu wa kuhubiriwa mpaka aje Tanzania."Alisema 
 
Pia Bwana Edwin aliongeza kuwa"Nimeamua kusema haya kwa sababu Nimewahi kushuhudia mchungaji wa Kanisa Fulani kutoka nje ya nchi alikuja hapa kwa lengo la kuhubiri ,baada ya mkutano wa mahubiri kumalizika kama ilivyopangwa aling'ang'ania kukaa hapa nchini.Ndipo ujue kuwa Tanzania ni kuzuri watu wanatamani Kukaa"
 
Aidha Afisa huyo wa uhamiaji amewataka wananchi wa jiji la Dodoma kushirikiana na idara ya uhamiaji kuwabaini watu wanaofanya  kazi za majumbani kutoka nje ya nchi bila kibali maalum  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
 
Alisema"Kuna baadhi ya watanzania wamekuwa wakiwatumikisha  kazi za ndani wasichana wadogo kutoka nje ya nchi kwa kigezo cha gharama nafuu.Naomba tushirikiane ili tuweze kuwabaini "
 
Kwa upande Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dodoma mjini ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo  Mhe:Patrobass Katambi amesema kuwa suala la ulinzi na usalama ni la kila mtu hivyo jamii inapaswa kulinda mali ya mwenzake.
 
"Suala la ulinzi na Usalama ni la kila mtu ,wana Dodoma tushirikiane kulinda mali ya mwenzake"Alisema .
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking