Donderdag, September 06, 2018

TACOGA: Utandawazi umeharibu maadili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu


Na James Timber, Mwanza
Chama cha Ushauri wa wanafunzi vyuoni (TACOGA) wametakiwa kuwaelimisha viongozi katika ngazi mbalimbali ya uongozi vyuoni, lengo likiwa kuepukana na changamoto za wanafunzi wanaofeli kutokana na kupungukiwa maadili mema pamoja na utandawazi.

Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi, Anthony Kondola kwenye Semina ya Washauri wa Wanafunzi vyuoni (TACOGA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru jijini Mwanza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa (TACOGA), Amina Mdidi alisema kuwa wamekutana kubadilishana mawazo na kuzitatua changamoto kwa kushirikiana na watoa mada kisha kutembelea baadhi ya vyuo jijini hapa.

''Wanafunzi waliopo vyuoni wamezungukwa na matatizo mbalimbali, ili wapate ahueni ya kutatua changamoto zinazowakabili lazima wafike katika ofisi ya mshauri ambayo inapatikana chuoni kwa ajili ya kushauriwa na kurudi katika hali yake ya kawaida ikiwa ni pamoja na kuongezewa ujuzi zaidi itakayowafanya waweze kufaulu vizuri masomo yao,'' alisema Mdidi.

Aidha Katibu Muenezi wa (TACOGA), Zitta Mnyanyi alisema kuwa wamekuwa na malengo mengi lakini lengo kuu ni kutoa ushauri na maelekezo kwa wanafunzi kwa kufuata kanuni  taratibu, ili mwanafuzi amalizapo chuo aweze kuishi katika jamii na kuisaidia kufikia  malengo mbalimbali.

Mnyanyi, alisema kuwa toka waanzishe chama hizo wamepiga hatua kwa asilimia kubwa ya malengo waliokuwa nayo ikiwemo kupunguza migomo vyuoni pia wanafunzi wamekuwa wakinufaika na mambo mengi kuhusu elimu waipatayo  kutokana na washauri kuongeza ujuzi kupitia zaidi kupitia midahalo, semina mada mbalimbali pale wanapokutana na katika chama chao.




mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking