Woensdag, Februarie 07, 2018

Trump aiambia Pentagon iandae gwaride la jeshi Washington



Donald TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kuwauliza maafisa wakuu wa jeshi kuandaa gwaride kubwa zaidi nchini humo kuonyesha nguvu zake za kijeshi.
Afisa anayehusika na masuala ya habari katika ikulu ya white house, Sarah Sanders amesema rais Trump amewaagiza wakuu wa jeshi kupanga hafla hiyo ambayo raia wa taifa hilo watatoa shukrani na heshima zao kwa wanajeshi wao.
Ripoti zinasema kuwa rais Trump alifurahishwa mno na sherehe za Bastille nchini Ufaransa, ambako mbali na wanajeshi kuonyesha wanajeshi wake, magari ya kivita na vifaru pia inajumuisha maonyesho ya ndege za wana anga.
Sasa rais Trump anataka Marekani kuiga mfano huo wa Ufaransa.
Sherehe ambayo anasema itafana zaidi kuliko ya Ufaransa.
Kufuatia agizo hilo maafisa wakuu wa idara ya ulinzi nchini Marekani kwa sasa wanatafakari pendekezo hilo.
Suala muhimu ni tarehe ya sherehe hizo.
Siku ya kuwakumbuka wakongwe wa kivita huadhimishwa tarehe kumi na moja Novemba kila mwaka na inasemekana huenda sherehe hizo zikaandaliwa siku hiyo.
Tayari maeneo matatu ambayo huenda yakafikiriwa kuandaa sherehe hizo yametolewa.
Rais Trump anasemekana kupendekeza sherehe hizo kuandaliwa katika barabara ya Pennsylvania inayoliunganisha bunge la congress na ikulu ya white house na hoteli ya Trump International.

Jeshi la MarekaniHaki miliki ya pichaREUTERS

Lakini kuna wasi wasi kuwa baada ya sherehe hizo bara bara hiyo huenda ikaharibiwa kabisa kutokana na uzito wa vifaa vya kijeshi.
Tamasha za kijeshi sio za kawaida nchini Marekani kwa sababu ni ghali.
Sherehe za mwisho za kijeshi kuandaliwa baada ya vita vya ghuba iligharimu serikali dola milioni kumi.
Je ni kila mtu ana ridhia pendekezo hilo?
Wanasiasa wa chama cha Democratic wameshutumu mpango huo kwa gharama kubwa na kusema kuwa fikra hizo zinatoa ishara za kutia wasiwasi.
"Ni njia ovyo ya kupoteza fedha!" alituma ujumbe wa twitter mwakilishi Jim McGovern. "Trump anaonekana kuwa dikteta zaidi ya rais , Wamarekani wanastahili kiongozi bora zaidi."
Mwakilishi Jackie Speier, ambaye ni mwanachama wa kamati ya bunge kuhusu huduma za kijeshi ameliambia shirika la utangazaji CNN: "Nilishangazwa na pendekezo hilo kwa kweli .... tuna kiongozi anayetaka kuwa kama Napoleon."
"It's really a waste of money, and I think everyone should be offended by his need to always be showy... it's not our style, it's not the way we do business."

Chrispiny kalinga blog

Tetemeko la ardhi laangusha Maghorofa na kuua



Taarifa katika vyombo vya habari vya kimataifa leo February 7, 2018 ni kuhusiana na tukio lililotokea katika mji wa

“Hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa mwanzo” –Nape Nnauye





Tokeo la picha la nape nnauye

Mkutano wa Bunge la kumi umeendelea Dodoma ambapo Wabunge walikuwa wakichangia mapendekezo yao

ZUMA azuiwa kutoa hotuba Bungeni


Spika wa Bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete amesema hotuba ya kila mwaka ya Rais Jacob Zuma ambayo ingeelezea  kuhusu hali ya nchi, imeahirishwa kutokana na mashinikizo anayokabiliana nayo Rais huyo

Swansea yaiua Notts County 8-1 FA CUP.



Tammy AbrahamHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTammy Abraham
Michuano ya FA CUP imepigwa Jana usiku kwa michezo mitatu, Swansea city wakafanikiwa kuwabamiza Notts County kwa kichapo cha mabao 8 -1

Conte: naiachia klabu ifanye uamuzi

epl


Haki miliki ya pichImage caption
Meneja wa Chelsea Muitaliano,Antonio Conte, baada ya kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya Watford amesema anaiachia klabu yake kufanya uamuzi kama wanafikiri hafanyi kazi nzuri.

Bondia Muhammad Ali afungiwa miaka miwili



BoxingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBondia Muhammad Ali amefungiwa kwa miaka miwili
Bondia Muhammad Ali, raia wa uingereza amefungiwa kwa miaka miwili kujihusisha na mchezo wa masubwi baada ya kushindwa vipimo vya dawa zilizokatazwa michezoni.

Misri yamchunguza mnenguaji kwa 'kuchochea maadili mabovu'


Misri yamchunguza mnenguaji kwa 'kuchochea maadili mabovu'
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMisri yamchunguza mnenguaji kwa 'kuchochea maadili mabovu'
Misri yamchunguza mnenguaji kwa 'kuchochea maadili mabovu'
Mashtaka dhidi ya Ekaterina Andreeva yapo pamoja na "kuvaa nguo zinazokiuka vigezo vilivyowekwa"

Trump aiambia Pentagon iandae gwaride la jeshi Washington


Donald TrumpHaki miliki ya picha
Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kuwauliza maafisa wakuu wa jeshi kuandaa gwaride kubwa zaidi nchini humo kuonyesha nguvu zake za kijeshi.

Mkutano wa kumjadili Zuma waahirishwa leo



Rais Jacob Zuma na shinikizo la kuachia madaraka
Image captionRais Jacob Zuma na shinikizo la kuachia madaraka
Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.

Nuh Mziwanda atoa ya moyoni baada ya wimbo wake kuvuja

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta akihuzunishwa na kitendo cha wimbo wake kuvuja kwani hakuwa na mpango wa kuutoa sasa hivi.

Mimi Mars afunguka mahusiano yake na Jux

MIMI Mars ni miongoni mwa wanadada wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva. Jina lake alilopewa na wazazi wake ni Marianne Mdee na ni mdogo wa damu wa mwanamuziki Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Prof. Kabudi asema hakuna mgongano wa Katiba Bara na Visiwani

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema hakuna mgongano mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar unaosababisha ongezeko la kero za Muungano.