Donderdag, Februarie 22, 2018

Msajili wa vyama aiandikia barua Chadema

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Ubalozi wa Marekani Montenegro washambuliwa

Ubalozi wa Marekani mjini  Podgorica   washambuliwa kwa bomu lilitengenezwa kienyeji  kwa mikono  nchini Montenegro.

Mwili wa Akwilina ulivyochukuliwa Muhimbili kupelekwa NIT kuagwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliongoza msafara wa magari, likiwemo lililobeba mwili wa  mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuagwa.

Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi lilikuwa  katika gari maalumu la kubebea maiti.

Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi itaanza. Akwilina atazikwa kesho 


Chrispiny kalinga blog

Wanafunzi Wazimia na Kupoteza Fahamu Baada ya Kumuona Akwilina ndani ya Jeneza

Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.

Mpenzi Wangu Ibilisi ( Simulizi ya Kweli) Sehemu ya 01

Mwandishi: Grace Godfrey Rweyemam
“Habari dada Grace! Ninaweza kuonana na wewe tuongee?”
Nilipata ujumbe huo mfupi wa simu kutoka kwa namba nisiyo ifahamu nikiwa katikati ya shughuli zangu.

Taarifa Muhimu Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusimamia vizuri rasilimali walizonazo na kukusanya kodi vizuri ili waweze kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu na kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Woensdag, Februarie 21, 2018

Kipindupindu chaua 18 Dodoma



Watu 18 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mkoani Dodoma ndani ya miezi minne huku zaidi ya watu 470 wakiugua ndani ya muda huo.

Rais Magufuli awasili SALAMA Nchini Uganda

Rais John Magufuli leo amewasili nchini Uganda, kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaofanyika  mjini Kampala.

Ni kosa polisi kujichunguza kwa Matukio yanayowahusu”......Hili ni Tamko la Asasi za Kiraia Kuhusu Hali ya Usalama Nchini


WITO WA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU HALI YA USALAMA WA RAIA, HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA WA SHERIA NCHINI

UTANGULIZI
Sisi Asasi za Kiraia tulioweka sahihi katika Waraka huu, kwa umoja wetu tumesikitishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala wa sheria na usalama wa raia vinavyoendelea hivi

Serikali Yaridhia Gharama za Mazishi ya Akwilina....Yagoma Kutoa fedha taslim


Wednesday, February 21, 2018

Serikali Yaridhia Gharama za Mazishi ya Akwilina....Yagoma Kutoa fedha taslim

Familia ya marehemu  Akwilina Akwiline inaendelea na maandalizi ya mazishi, huku ikielezwa kuwa Serikali imekubali kuyagharimia lakini si kutoa fedha.

Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Misungwi Na Mwanasheria Wakamatwa

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana  na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa  imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere Akifafanua Lengo halisi la Mkutano huo,
Na Maiko Luoga Ludewa. 
Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Mh, Andrea Tsere Amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Ambao Shule zao Zimeshika Nafasi za Mikia zilizopo Katika Makundi ya Shule Kumi Duni Kwa matokeo ya Darasa la Saba na kidato cha Nne mwaka 2017 Wajiudhuru Nafasi zao za Ukuu wa Shule kwakuwa Wameshindwa Kutekeleza Majukumu yao.

TAZAMA LUDEWA KUPEWA UTARATIBU MWINGINE

Mbunge Wa Ludewa Mh, Deo Ngalawa Akichangia Mjadala Wa Elimu Jana,