Woensdag, Februarie 28, 2018

UN: Mapigano yamezuia kusambaza misaada Ghouta, Syria

Umoja wa mataifa umesema mapigano yanayoendelea Mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria yamezuia kusambazwa kwa misaada licha kukubaliana kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano kwa saa tano.

Trump amtaja Parscale kama meneja wa kampeni zake za 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020.

Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni

Atiwa mbaroni baada ya kutekeleza mauaji katika Facebook live

Prentis Robinson alifariki akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja ya facebook Live

Maafisa wa polisi kaskazini mwa Carolina wanasema kuwa mtu mmoja alipigwa risasi hadi kufa alipokuwa akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja katika mtandao wa facebook Live

Yanga yapewa muda wa kuimaliza Botswana


YANGA kwa sasa watakuwa na uhakika wa kuwamaliza wapinzani wao, Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa hapa nyumbani baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwafutia mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Shilole na mumewe wasaka mtoto

STAA wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita kwa sasa yeye na mumewe, Ashraf Uchebe wako kwenye harakati za kusaka mtoto.

Jenerali Mabeyo asema kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.

Yanga yapewa majina ya wachezaji hatari wa Botswana

TIMU ya Yanga, imepewa majina matatu ya nyota wanaokipiga kwenye kikosi cha Township Rollers ya Botswana ambao wanatakiwa kuwachunga ili wasiweze kuwaletea

Hii ndio ripoti ya idadi ya Watu Tanzania


Ripoti ya makadirio ya watu nchini inaonyesha Tanzania kuna idadi ya watu 54.2 milioni hadi kufikia mwaka 2018 huku ikieleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6.

Waziri Mavunde aagizi Wakurugenzi kupandishwa Kizimbani



NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.

Daktari wa Simba SC azungumzia hali ya Okwi


Daktari wa klabu ya Simba, Yassin Gembe amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anaendelea vizuri kufuatia majeraha aliyopata kwenye mchezo uliyopita dhidi ya Mbao FC.

Heri Muziki afunguka hataki tena kuwa katika Mahusiano na mtu maarufu


Muimbaji wa Bongo Flava, Heri Muziki amesema baada ya kuachana na aliyekwa mpenzi wake, Diva hatarajii tena kuwa katika mahusiano na mtu maarufu.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Cheche’ ameimbia Bongo5 kuwa baada ya kuachana na Diva ndio itakuwa mwisho wa yeye kuingia katika mahusiano na mtu maarufu.

TCRA yasitisha nyimbo zisizokuwa na maadili




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] imepokea Orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa [BASATA].

Kenya: Kiongozi wa wanafunzi auawa kwa kupigwa risasi

Kifo cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Kenya kimezuaa shutuma mpya za mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi nchini humo.