Umoja wa mataifa umesema mapigano yanayoendelea Mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria yamezuia kusambazwa kwa misaada licha kukubaliana kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano kwa saa tano.
Prentis Robinson alifariki akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja ya facebook Live
Maafisa wa polisi kaskazini mwa Carolina wanasema kuwa mtu mmoja alipigwa risasi hadi kufa alipokuwa akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja katika mtandao wa facebook Live
YANGA kwa sasa watakuwa na uhakika wa kuwamaliza wapinzani wao, Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa hapa nyumbani baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwafutia mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.
STAA wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita kwa sasa yeye na mumewe, Ashraf Uchebe wako kwenye harakati za kusaka mtoto.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.
TIMU ya Yanga, imepewa majina matatu ya nyota wanaokipiga kwenye kikosi cha Township Rollers ya Botswana ambao wanatakiwa kuwachunga ili wasiweze kuwaletea
Ripoti ya makadirio ya watu nchini inaonyesha Tanzania kuna idadi ya watu 54.2 milioni hadi kufikia mwaka 2018 huku ikieleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.
Daktari wa klabu ya Simba, Yassin Gembe amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anaendelea vizuri kufuatia majeraha aliyopata kwenye mchezo uliyopita dhidi ya Mbao FC.