Vrydag, Maart 09, 2018

Rais Kenyatta na Odinga wakutana....waapa kufanya kazi pamoja

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa NASA Raila Odinga leo March 9, 2018 wamekutana rasmi na kuzungumza.

Rais Magufuli Aahidi kumpa Kazi Dr Kimei wa CRDB



Rais John Magufuli amesema licha ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei anakaribia kustaafu ameahidi kumpatia nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano.

HAWA WANAOUAWA SIO WATANZANIA, SIWEZI KUJIUZULU


































Chrispiny kalinga blog

Mwigulu Nchemba: Hakuna Tishio Lolote la Watu Kutekwa au Kuuawa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema Tanzania hakuna tishio lolote kuhusu watu kupotea au kuuawa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kusema kuwa Wizara yake inapambana kuhakikisha watu na mali zao wako salama. 

Mahakama yamuagiza AG kujibu kesi zinazohoji kukatazwa maandamano

Na Regina Mkonde

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuleta majibu kuhusu mashauri mawili ya kikatiba yaliyofunguliwa mahakamani hapo na wanaharakati dhidi ya ofisi yake, ifikapo Machi 21 mwaka huu.

Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kali Kwa Waliopanga Kuandamana.......14 Watiwa mbaroni mauaji makada wa Chadema

KAMISHNA wa Operesheni wa Polisi (CP), Nsato Marijani amesema hadi sasa watuhumiwa waliokamatwa kudaiwa kuhusika na kifo cha Kada wa Chadema, Daniel John wamefikia wanne.

Rais Magufuli: Hii Vita ni Kubwa Sana, Watanzania Tuungane Pamoja

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema suala la maendeleo linapigwa vita sana hivyo amewataka watanzania waunge mkono hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ili kuweza kuimarisha uchumi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Woensdag, Maart 07, 2018

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Mjini

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kaburu kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 07 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dkt. Walid Amani Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu”

Hii ni sehemu ya salamu za rambirambi alizotuma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kaburu.

Pamoja na salamu hizo Mhe. Rais Magufuli ameiombea familia ya Marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi na amemuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
07 Machi, 2018

Chrispiny kalinga blog

Nape afunguka kuhusu Bashe

Mbunge wa Mtama (CCM) Ndugu Nape Nnauye amewataka Wabunge wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono Mbunge Hussein Bashe juu ya hoja yake binafsi aliyoiwasilisha kwa Katibu wa Bunge.

Nguvu ya Dhaifu - Sehemu ya 02 ( Simulizi ya Kweli)


Mwandishi: Grace G. Rweyemam

Nilipofika nje kule walikokuwa wakicheza watoto, nilikuta Karitta ameanguka chini na mate yanamtoka, mwili umekakamaa.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) adaiwa kutoweka Katika mazingira Ya Kutatanisha

Taarifa zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) atuma salamu za rambirambi




Chrispiny kalinga blog

Dinsdag, Maart 06, 2018

Makonda - Sitaki Kuona mwananchi wa Dar akiteseka

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameitaka bodi ya barabara kuhakikisha fedha za Mkopo wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara DMDP zinatumika kujenga Barabara za kisasa na sio kutumika kwenye Warsha, Semina na Safari za Mafunzo Nje ya Nchi ambapo Mwisho wa siku fedha hiyo inamalizika bila kufanya jambo lililokusudiwa.