Woensdag, Augustus 01, 2018

NDOA YA ERICK MLELWA YAAMSHA MENGINE MKOANI NJOMBE

Huyu kushoni ni bibi harusi na kulia ni msimamizi wa bibi harusi

TRA yawasha moto usio zima...



Na Chrispin Kalinga

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewaagiza mameneja wake wote nchini kufanya operesheni sehemu za biashara baada ya kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatoi risiti za kielektroniki za EFD kwa kisingizio cha mfumo.

Zari Anena mazito

 Baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amekuja juu na kumwaga povu zito siku ya jana na kuomba asilinganishwe na vinuka mkojo.

Baba afunguka Samatta kwenda Leicester City


ACHANA na habari za La Liga. Straika namba moja wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anaweza kuwashangaza mashabiki wake kwa kutua Ligi Kuu ya England muda wowote kuanzia sasa.

Jeshi la Polisi Lasema Mbwa Aliyedaiwa Kupotea Alikuwa Kwenye Mafunzo

Na Chrispin Kalinga

Mbwa wa kazi maalum za Bandari ya Dar es Salaam anayedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, alikuwa kwenye mafunzo bwalo la Polisi.

Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Aliowateua......Asema Ilimlazimu Kukaa na Majina yao Miezi Minne Akiwachuja

Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.

Maandag, Julie 30, 2018

OFA MAALUM KWA WATANZANI KIJANA CHANGAMKIA



Mkuu wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ECKROS kilichopo mkoa wa NJOMBE anayo furaha kuwa julisha wale wote walio hitimu kidato cha nne kuwa chuo kinapokea maombi kwa ajili ya kujiunga na kozi zifuatazo:-
1.   Uandishi wa Habari na Utangazaji  (Radio na TV)

Mugabe amtosa Mnangangwa, asema kura yake anaipeleka upinzani

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema hamuungi mkono mrithi wake Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa ndani ya chama tawala Zanu PF, kwa kile alichodai kuondolewa kwa nguvu madarakani na chama alichokianzisha.

Waziri Lugola Kuyafuta Makanisa Na Misikiti Yenye Kuendeleza Migogoro Na Kutofuata Sheria Za Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema hatasita kufuta makanisa au misikiti inayoshindwa kutatua migogoro ya taasisi hizo.

Waziri Mkuu: Wanaowapa Ujauzito Wanafunzi Kupewa Adhabu Kali

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka sheria kali zinazowalinda  watoto wa kike na watakaobainika kuwapa ujauzito na kukatisha masomo yao adhabu watakayoipata hawatoisahau maisha.

TFDA Yatakiwa Kusajili Jengo La Uzalishaji Chakula Ndani Ya Siku 10.


NA WAMJW- DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutoa kibali cha kusajili jengo la kuzalisha bidhaa za chakula ndani ya siku kumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha wadau kujadili mchango Taasisi za Serikali katika kuanzisha na kuboresha viwanda vya Chakula nchini leo jijini Dar es salaam.

"Naielekza TFDA kutoa kibali cha kusajili jengo la kutengeneza bidhaa za chakula ndani ya siku 10 pamoja na siku 30 za kusajili bidhaa husika ili kuleta chachu ya maendeleo ya viwanda nchini" alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy ameitaka TFDA kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa za vyakula kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya sayansi juu ya uzalishaji bora wa vyakula na wenye tija kwa wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amewataka TFDA kutopunguza viwango vyao vya ukaguzi wa bidhaa za vyakula ili kuleta sifa na ushindani kwenye soko la kimataifa.

"Nazitaka Taasisi za Serikali ikiwemo TFDA, TBS, MKEMIA MKUU WA SERIKALI na taasisi ya Mionzi kushirikiana katika kudhibiti ubora wa bidhaa nchini na kupunguza vikwazo kwa wawekezaji wa viwanda vya chakula nchini" alisema Waziri Mwijage.

Aidha Waziri Mwijage amewataka wajasiliamali wasibweteke katika kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango kwa mahitaji na zenye kulinda afya za watanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Sitta Kijo amesema kuwa wamejidhatiti kuhakikisha hawatokuwa vikwazo kwa wawekezaji katika sekta ya uwekezaji kwenye viwanda vya chakula nchini.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Dkt. Edward Sembeye ameipongeza TFDA kwa kupunguza malalamiko na vikwazo vingi kwa wajasiliamali na wawekezaji wadogo wa vyakula hapa nchini.

mubashara blog +255753121916

Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Mwaka Huu

Rais John Magufuli amesema atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi serikali yake kuhamia huko.

Kauli ya Ndugai baada ya Waitara kujiuzulu

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema amepokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara ya kujivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu wadhifa huo.