Donderdag, April 26, 2018

Wahanga wa mafuriko Jangwani wapata neema...tizama video live hapo chini



Familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na

India: Wanafunzi 14 wafariki katika ajali ya treni

Watu 14 wafariki katika ajali ya treni iliotokea baada ya kugonga basi la wanafunzi Uttar

Boti yapinduka Ziwa Victoria

Watu wawili wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kupinduka. Ilipokumbwa na dhoruba kali katika ziwa Victoria, Sengerema jijini Mwanza.

Akizungumza na www.eatv.tv kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema boti hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao walikuwa wa wakisafiri kutoka Sengerema kuja Mwanza, na ndipo ilipokumbwa na dhoruba wakiwa njiani, na kusababisha boti hiyo kupinduka na watu hao kufariki.

“Kuna boti ilikuwa inatoka Sengerema kuja huku Mwanza, ilikuwa imebeba mkaa pamoja na udaga, walivyokwenda kama robo safari yao hali ya hewa ikawa mbaya kukawa na dhoruba, wakiwa wanageuza wanarudi ikawa shida ikapinduka, ndani ya hiyo boti kulikwa na watu watano, wanaume wanne mwanamke mmoja, watatu waliweza kuogelea lakini hawa wawili walishindwa, mwanamke na mwanaume mmoja, majina bado sijayapata”, amesema Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi amesema miili ya watu hao imepatikana, na wanafanya utaratibu wa kuihifadhi hospitali, ili ndugu waweze kuitambua na kuichukua kwenda kuzika.
Chanzo cha habari muungwana.


mubashara blog +255753121916

Mzee Kilomoni atoa nasaha zake kwa Simba kuelekea mechi dhidi ya Yanga Jumapili hii.

Mwanachama aliyesimamishwa na uongozi wa klabu ya Simba kufuatia sekeseke la kufungua kesi mahakamani kupinga mabadiliko, Mzee Hamis Kilomoni, ametoa nasaha zake kwa Simba kuelekea mechi dhidi ya Yanga Jumapili hii.

Simba yawasili Dar

SIMBA SC tayari wapo mjini Dares Salaam tangu mchana kwa maandalizi ya mwisho ya pambano dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumapili Uwanja wa Taifa.

Mzee Akilimali afunguka kuhusu Yanga

Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameomba wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuendeleza umoja ndani ya timu yao ili iweze kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Simba.

Kauli ya Balozi Dkt Slaa kuhusu Watanzania walioandamana nchini Sweden

Wakati polisi wakitoa tahadhari kwa wananchi kuhusu maandamano yaliyoratibiwa kwenye mitandao ya kijamii na kupangwa kufanyika leo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa amesema ofisi yake ilipokea barua kutoka polisi wa nchi hiyo kuhusu taarifa za Watanzania waliotaka kuandamana jana.

Hali ya Usalama Iringa Iko Shwari.....Diwani mmoja Katiwa Mbaroni


Na chrispin kalinga

Hali ya usalama mkoani Iringa leo imeendelea kuwa shwari licha ya tishio la maandamano yaliyotarajiwa kuwepo huku ulinzi ukiimarishwa katika baadhi ya maeneo yenye mkusanyiko mikubwa kama benki na vyuo vikuu.

Rais Magufuli: Anena mazito : Tutawashughulikia wote watakao uchezea Muungano ...awe Nje ya Nchi au Ndani ya Nchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi.

Rais Magufuli Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 3319....swali lipo je lulu atabahatika.jisomehe mwenyewe

Rais Magufuli  katika kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa 3,319 ambapo wafungwa 585 wataachiwa huru leo, na 2,734 wamepunguziwa adhabu zao.

9 mbaloni wakiandamana Posta, Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta.

Wema amuweka mdomo wazi Mange Kimambi kuhusu maandamano yake...

NA CHRISPIN KALINGA

Wema Sepetu amempiga dongo Mange Kimambi kufuatia maandamano aliyokuwa akiyahamasisha kupitia mitandao ya kijamii akiwataka Watanzania waandamane kutokufanikiwa.

Mambosasa AWASHA MOTO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea ufafanuzi suala ambalo limeanza kushika hatamu mitandaoni la kukamatwa kwa Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA kata ya Kisutu Elizabeth Mambosho na kupelekwa rumande akiwa na mtoto mchanga.