Saterdag, November 25, 2017

LUDEWA 
HILI NALO NENO

Na chrispiny kalinga

Ili kuhakikisha lengo la serikali ya awamu ya tano Kufikia Tanzania ya viwanda linatimia Baadhi ya viongozi Mkoani Njombe Wameanza kumuunga mkono Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Kwa vitendo.
Mh, Neema Mgaya ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa njombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM ameamua kutoa msaada wa Vyerehani 370 kwa vikundi vya wanawake wa mkoa wa Njombe vyenye zaidi ya Tsh, Milioni 90 ambavyo ni sawa na viwanda vidogovidogo zaidi ya 90 kwakuwa Vyerehani vinne ni sawa na kiwanda kidogo kimoja.
Akiwa wilayani Ludewa November 24 mwaka huu Mh, Neema Mgaya Alikabidhi vyerehani 64 kwa vikundi vya wanawake wa Tarafa za Liganga, Mawengi, Mlangali, Masasi, na Tarafa ya Mwambao pamoja na Kukabidhi vifaa vya Michezo kwa timu ya wanawake ya Mapinduzi Queens Ambayo ni Bingwa wa Mkoa wa Njombe.
Aidha Mbunge huyo wa Viti maalumu pia Alimkabidhi Afisa Elimu wa shule za sekondari wilaya ya Ludewa bw, Matenus Ndumbaro Vitabu vya Masomo ya ziada kwa shule 23 za sekondari zilizopo ndani ya wilaya ya Ludewa ambazo ni za Serikali pamoja na Shule za Binafsi kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi kuongeza Maarifa kwa Muda wa ziada.
Kwaupande wake Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh, Josephat Kandege aliyefika wilayani Ludewa Kumuunga mkono Mh, Neema Mgaya Alimpongeza Mbunge huyo kwa uamuzi huo alioufanya wa kuwainua kiuchumi wanawake wa Mkoa wa Njombe.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking