Donderdag, April 26, 2018

India: Wanafunzi 14 wafariki katika ajali ya treni

Watu 14 wafariki katika ajali ya treni iliotokea baada ya kugonga basi la wanafunzi Uttar Pradesh nchini India
Watu 14 wamefariki katika ajali iliotokea katika jimbo la Uttar Pradesh  nchini India. Ajali hiyo imetokea baada ya basi la lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi kugongana na treni.

Vyanzo vya habari katika eneo hilo vimeafahamisha kuwa miongoni mwa wanafunzi 22 waliokuwa  katika basi hilo, 13 walifariki wakati wa tukio.

Watu wanane wamejeruhi huku wanne miongoni mwao wakiwa wamejeruhiwa vikali. Sababu zilizopelekea ajali hiyo bado hazijafahamika

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking