Maandag, April 09, 2018

Adhabu ya Kifo Mali, yashutumiwa

Kikundi cha kutetea haki za binaadamu nchini Mali kimeshusha mzigo wa lawama kwa jeshi la nchi hiyo kutokana na kitendo cha kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa kumi na wanne katikati mwa jiji la Dioura.

Jeshi la nchi hiyo liliarifu kuwa wafungwa hao walikamatwa Almamisi wiki iliyopita na kuuawa muda mfupi tu baadaye.

Ndugu wa marehemu, ambao wanatoka katika kundi la kabila la Fulani, wametoa maelezo kuwa, ndugu zao hawakuwa na nasaba yoyote na makundi ya vijana wenye msimamo mkali.

Jamii hiyo ya kabila la Fulani imelalamika kuwa hii si mara ya kwanza kuhusishwa na makundi yenye msimamo mkali wa kidini.

Wiki hii, harakati za kundi la haki za binaadamu la Amnesty International limearifu kuwa wanaume sita walikutwa wamekufa katika kaburi la halaiki mapema mwezi uliopita ambao walitiwa mikono na jeshi siku tatu nyuma.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking