Dinsdag, April 10, 2018

Tanzania yazindua chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi

Binti akionyesha kadi yake baada ya kupokea chanjo
Image captionBinti akionyesha kadi yake baada ya kupokea chanjo
Serikali ya Tanzania imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.
Zaidi ya wasichana laki 6 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14 watachanjwa nchini nzima.
Msichana akionesha kadi yake ya chanjo
Image captionDuniani, kuna zaidi ya wanawake 260,000 wanaofariki kwa sababu ya saratani ya shingo ya kizazi
Huenda chanjo hii ikawakomboa wanawake na wasichana wengi kama wakijitokeza na kupata chanjo mapema zaidi.
"Saratani ya shingo ya kizazi ndio inayojitokeza zaidi Tanzania na ni chanzo cha vifo na magonjwa yanayohusiana na saratani miongoni mwa wanawake nchini."meneja wa mradi Daphrosa Lyimo aliiambia BBC.
Msichana mmoja akiandikishwa katika zoezi la uzinduzi
Image captionMsichana mmoja akiandikishwa katika zoezi la uzinduzi
"Duniani, kuna zaidi ya wanawake 260,000 wanaofariki kwa sababu ya saratani hii, ambayo inazuilika na inatibiwa ikigunduliwa mapema." aliongezea Bwana Lyimo
Serikali ina matumaini kuwa kampeni hiyo itapunguza gharama za afya. Kumuuguza mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kunaweza kugharimu takriban dola za Marekani elfu 2 wakati dola 15 zitatumika kuwachanja wasichana maafisa walisema.

Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:

  • Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote
  • Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
  • Kula chakula chenye afya
  • Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
  • Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
  • Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
  • Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba
  • Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
  • Punguza unywaji wa pombe
  • Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking