Saterdag, April 21, 2018

Zari amlilia Masogange

WASANII  na watu mbali mbali wenye ukaribu na tasni ya burudani wameendelea kutoa  salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, Zari The Boss Lady naye hajakaa kimya.

Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia mtandao wa Snapchat Zari ameandika;

"We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis."  

Kwa kiswahili;
“Hatukuwa marafiki sana lakini tangu upate namba yangu umekua ukinitumia meseji kila mwezi na hakuna mwezi uliopita haujauliza kuhusiana na watoto wanaendeleaje pumzika kwa amani dada”

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking