Maandag, April 09, 2018

Njombe Mji FC yazidi kupunguza ubora wake.

Kivumbi cha Ligi Kuu Bara kiliendelea tena jioni ya jana kwa viwanja vinne kuwaka moto.

Katika mchezo uliopigwa huko Shinyanga, wenyeji Stand United walitoa dozi ya mabao 3-1 dhidi ya Njombe Mji FC kutoka Njombe.

Mbao ya Stand United yalifungwa na Suleiman Ndikumana katika dakika ya kwanza ya mchezo huku mengine yakitiwa kimiani na Sixtus Sabilo kwenye dakika za 84 na 90. Bao pekee la Njombe Mji lilifungwa na Notkelly Masasi katika dakika ya 75.

Wakati huohuo Kagera Sugar ililazimisha sare ya mabao 1-1 dhidi ya Ndanda FC katika dimba la Nangwanda Sijaona huko Mtwara, Ndanda walijipatia bao lao kupitia Mrisho Ngassa (33') na Kagera wakijipatia goli kupitia Abdallah Mguhi ( 27').

Matokeo ya mechi zingine yalikuwa ni suluhu ya 0-0 kwa Mbeya City iliyoikaribisha Azam FC huko Mbeya, Sokoine Stadium. Ruvu Shooting nayo ikalazimishwa suluhu ya kutofungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking