Saterdag, April 21, 2018

UVCCM MKOANI NJOMBE YAWASHA MOTO KWENYE VYUO NA VYUO VIKUU HUKU CHADEMA WASHIKWA NA BUTWAA.


Na Chrispiny Bernad Kalinga.
Njombe.

Aliye simama ni Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Njombe Emmanuel mlelwa katika Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Njombe na kushoto kwake ni Katibu Mwenezi Siasa Mkoa wa Njombe Muheshimiwa Erasto Ngole.


 
Umoja wa vijana Uvccm  vyuoni Mkoani Njombe wamefanya kikao cha pamoja kwa muunganiko wa vyuo na vyuo vikuu vilivyopo katika mkoa huo kwa lengo la kuwekana sawa na kukijenga chama cha mapinduzi.

Sambamba na hayo wanavyuo hao wamefanikiwa kuwasajili  wanachama wapya wasio pungua sabini na tatu kutoka katika vyama pinzani huku wengine wakiendelea kuingia kinywa kinywa ambapo wasomi hao wametokea katika vyuo:chuo cha Hagafilo,Mpechi vtc,Eckros School of Journalism,Amani na vinginevyo vingi.

Hata hivyo semeni hiyo imeendeshwa na viongozi wa mkoa huo akiwepo katibu mwenezi wa siasa mkoa huo mweshimiwa   Erasto Ngole na mwenyekiti Uvccm mkoan wa njombe mweshimiwa Erasto Ngole mwenyekiti seneti mkoa Emmanuel mlelwa katibu uvccm Shua Mwasanguti na katibu senita mkoa  getruda shungwa.

Sambamba na hayo mgeni rasmi wa semina hiyo mweshimiwa Erasto Ngole amewapongeza viongozi wa idara zote kwa kufanya kitu kizuri cha kuwakutanisha wasomi hao pamoja  na akaongeza kwa kusema kuwa wote walio jiunga na chama leo wasiludi nyuma  bali wazidi kusonga mbele na akaongeza kwa kumpongeza mwenkiti wa vijana wa mkoa kwa kumpa kama hongera kwa shilingi elfu hamsini papohapo.

Kwa upande wake  akamaliza kwa kusema kuwa anawaomba vijana wote waongeze juhudi kwa kufanya kazi na akawaonya watu wanaotaka kufanya maandamano siku zijazo kwa lengo la kupoteza amani na amesema kuwa vijana wasithubutu kuandamana bali wafanye kazi.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking