Sondag, April 08, 2018

Zaidi ya Wananchi 100 hawana makazi Msitu wa Tembo Simanjiro


Zaidi ya Wananchi 100 wa kijiji cha Msitu wa Tembo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na kusombwa na mafuriko ikiwemo ya mwenyekiti wa kijiji hicho kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali .

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Abel Mfuru amesema, zaidi ya nyumba 20 za udongo pamoja na vyoo vyake vimesombwa na mafuriko hayo na wananchi hakuna walichookoa katika nyumba hizo vikiwemo vyakula na nguo.

Bw .Mfuru ameiambia Muungwana Blog  iliyokwenda eneo la tukio kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha saa mbili za usiku na kuambatana na radi kali zaidi ya nne ambazo hata hivyo pamoja na mafuriko hayo hakuna aliyejeruhiwa.....insert ya bw abel mfuru mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha msitu wa tembo.

Wananchi walioathiriwa na mafuriko hayo  Bi. Maryana Hussein na Bw Paul Yohana ambayo yamesababishwa pia na kukatika kwa korongo moja ambalo lilizidiwa na maji wameiomba serikali msaada wa haraka wa chakula, mavazi na dawa ili wajikimu katika wakati huu na kujikinga na mlipuko wa magonjwa....insert ya wakazi wa kijiji cha msitu wa tembo.

Afisa Mtendaji wa kata ya Msitu wa Tembo Bw Selemani Mbacha amesema, wametoa taarifa za awali kwa uongozi wa wilaya hiyo na sasa wanafanya tathmini ya athari za mafuriko ikiwemo hasara na mahitaji halisi ya wananchi..



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking