Dinsdag, April 10, 2018

WAKULIMA LUDEWAWATAKIWA KUZALISHA PARACHICHI


Na Maiko Luoga Ludewa

Wakulima wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Wameshauriwa Kuzalisha Mazao ya Biashara kwa wingi yenye Fulsa za Soko la Uhakika ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania.




Wakitoa Ushauri huo kwa Wananchi wa Kijiji na Kata ya Luana Hapo jana Viongozi wa Mtandao wa Kilimo cha Matunda na Mbogamboga Wilaya ya Ludewa Akiwemo Bw, Jofrey Kayombo ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao huo Wilaya ya Ludewa Pamoja na Mratibu wa Mtandao Wilaya ya Ludewa Bw, Gidion Kayombo Wamesema kuwa Wakulima wanatakiwa Kuachana na Tabia ya Kulima mazao ya Chakula wakiamini kuwa ni ya Kibiashara.

Wakizungumza na Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Luana wilayani Ludewa waliojitokeza katika Mkutano wa Kuhamasisha Kilimo cha Tunda la Parachichi viongozi hao wamesema kuwa Wakulima wengi Wilayani Ludewa wamejikita zaidi katika Kilimo cha Mazao ya Chakula ikiwemo Mahindi na Maharage huku wakifikiri Kuwa mazao hayo ni Ya biashara na Kuishia kuilaumu Serikali pindi wanaposhindwa Kuuza mazao yao.

Wamelitaja Tunda la Parachichi Kuwa ni moja kati ya Mazao yenye Utajiri Mkubwa kwasasa Duniani kutokana na Uhakika wa Soko la zao hilo na Uhitaji wake Ni Mkubwa hivyo nvyema Wakulima wilayani Ludewa waanze Kuzalisha zao hilo kwa wingi zaidi.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Luana Bw, Adeliko Luoga Amewataka Wananchi katika Kijiji chake Kutambua kuwa Kilimo cha Parachichi katika Kijiji hicho ni lazima kwa Kila Mwananchi ili baada ya Mavuno wananchi wengi waweze Kujikwamua na Ugumu wa Maisha Unaowakabili.

Ugani na Mwenyekiti Luana
Katika Hatua nyingine Wananchi wa Kijiji Cha Luana wamesema kuwa Wameipokea Vyema Elimu hiyo ya Kuhamasisha Kilimo cha Parachichi Kwani wamekuwa wakizalisha Mazao Mahindi na Maharage Kwa Muda Mrefu tangu Kuumbwa kwa Dunia Bila Faida yeyote hivyo Wanaamini Kuwa Uwepo wa Mazao ya Biashara ni Mkombozi kwao kama wakulima.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking