Dinsdag, Januarie 30, 2018

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKAGUA STENDI MPYA NA SOKO NJOMBE,


Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitoa maagizo Kwa wataalamu wa Ujenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Akiwa Katika Stendi mpya Njombe Mjini. 
Kulia ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bw,Erasto Ngole Akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Katika Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Stendi mpya ya Magari Njombe mjini. 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitembelea na Kukagua maeneo mbalimbali Ndani ya Stendi Mpya ya Njombe, Mjimwema. 

Wakwanza Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri Aliyeambatana  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika Ziara hiyo. 
Nimwonekano wa baadhi ya Maeneo katika Stendi mpya ya Magari Njombe Mjini katika eneo la Mjimwema, 
Jengo la Vyoo na Bafu Katika Stendi Mpya ya Magari Njombe Mjini.

Na Maiko Luoga Njombe,
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Mapema Leo January 23 ,2018 Ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi Njombe Mjini Mradi ambao unaendelea kwakusuasua na Mkandarasi hayupo Saiti.

Baada ya kukagua Stendi hiyo ya mabasi Njombe, Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amebaini Kuwa kuta za Stendi hiyo zimejengwa Chini ya kiwango kwakuwa kabla ya Kuanza kutumika tayari Kuta hizo zimeshatengeneza Nyufa Licha ya Jengo hilo la stendi kutumia pesa nyingi za Serikali hatahivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amewaagiza Wataalamu wa Ujenzi Kuhakikisha Sehemu zote zenye matatizo zinarekebishwa na Hatua stahiki zakisheria Zinachukuliwa Kwa wote waliosababisha Upungufu huo wa jengo la Stendi mpya ya mabasi Njombe Mjini.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Wa Njombe pia Kwakuambatana na Uongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Njombe Bw. Hosea Mpagike na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Bw. Erasto Ngole kwapamoja wametembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Soko Jipya la Wafanyabiashara Mjini Njombe Kisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitoa maagizo Kwa Mkurugenzi wa mji wa Njombe Kuhakikisha ujenzi huo unakamilika Kwa haraka ili wafanyabiashara waweze kuendelea na Biashara zao.

Alipowasili Katika eneo la Soko kuu la wafanyabiashara Njombe mjini Mkuu wa Mkoa Hakuwakuta viongozi wa kata ya Njombe mjini na kupewa Maelezo kuwa viongozi hao wapo Katika kikao cha Kata ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Alitoa Amri kuwa Viongozi hao waache kikao chao maramoja na kisha wahudhurie mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe akizungumza na wafanyabiashara Katika soko kuu la wafanyabiashara Njombe Mjini.
Endelea kutembelea www.maikoluoga.blogspot.com Kwa Habari zaidi
chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking