Maandag, Januarie 29, 2018

Ndalichako amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Njombe

 LUDEWA

 NA CHARS IGINATO

Waziri wa Elimu sayansi,na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Njombe kwa jitihada zao na ushirikiano hasa kujiwekea utaratibu wa uchangiaji wa chakula cha wanafunzi mashuleni ili kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

W
aziri ndalichako ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wakazi wa shaurimoyo katika ziara ya kutembelea na kukagua chuo cha veta kinachojengwa na serikali kwa fedha zaidi ya shilingi Bilioni kumi ndipo alipofafanua juu ya kauli ya Rais Dr,John Pombe Magufuli aliyoitoa January 17 mwaka huu juu ya elimu bure

Aidha waziri huyo wa elimu ametumia nafasi hiyo kufafanua hatuba ya Rais Magufuli ya January 17 mwaka huu juu ya elimu bure ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi na walezi kuachana na wapotoshaji juu ya hotuba ya Mh,Rais.

Christopher Olesendeka ni mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye aliongoza msafara wa waziri huyo alipopewa nafasi ya kuzungumza aliiweka bayana mipango yake juu ya ujenzi wa chuo cha veta kinachojengwa shaurimoyo.


chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking