Dinsdag, Januarie 16, 2018


KUINGIA IKULU KWA MH.LOWASSA KWALETA GUMZO CHADEMA

Taarifa ya leo ya Edward Lowassa kuhusu alichoongea na Rais Magufuli IKULU




Leo January 15, 2018 Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ametoa taarifa inayoelezea mambo aliyoyajadili wakati alipokwenda IKULU kukutana na Rais Magufuli January 9 2018.

Baada ya kutoka IKULU hiyo January 9 Lowassa alisifia utendaji kazi wa Rais Magufuli kwa aliyoyafanya toka ameingia madarakani ambapo alitaka pia Watanzania waendelee kumuunga mkono.

Taarifa ya Lowassa ya leo inanukuliwa ikiwa imeandikwa yafuatayo >>> “Mnamo January 9 2018 nilipokea mwaliko kutoka kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli akiniomba kwenda kukutana nae IKULU siku hiyohiyo kwa ajili ya mazungumzo

Aidha, Jumapili January 14 2018 nilipata fursa ya kukielezea kwa kina Chama changu kupitia kikao cha kamati kuu ya mazungumzo yangu na Rais Dr. Magufuli IKULU, ujumbe wa Rais Magufuli kwangu ulikua ni kunishawishi nirejee CCM suala ambalo sikukubaliana nalo

Na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga CHADEMA haukuwa wa kubahatisha” – Edward Lowassa.

 

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking