Woensdag, Januarie 31, 2018

PEMBEJEO, MBOLEA CHANGAMOTO, LUDEWA,




                                                                


wakazi wa kijiji cha ludewa mjini katika wilaya ya ludewa wanaulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa madai ya kuletewa mbolea ya kukuzia mazao isiyo jitosheleza.

wakizungumza na mwandi wa habari juu ya uchache wa mbolea iliyo kuwa imeletwa katika kijiji hicho siku ya tarehe 28 mwezi huu ni mifuko mia moja na mbili tu ukilinganisha na wingi wa watu wa kijiji hicho.

hali kadhalika wananchi hao wameongeza kwa kusema kuwa licha ya mbolea hiyo kuuzwa kwa bei ya juu kwanzia sh.46000/=na wafanya biashara wengine huuza kwa sh.50000 lakini bado mbolea haitoshi na wakaiomba serikali kuongeza wingi wa mbolea katika wilaya hiyo. 

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya ludewa mh.Andrea Tsere amesema kuwa kwanzia siku ya kesho anawataka wafanya biashara wote kuleta mbolea ya kutosha na yeye ndiye atakaye toa kibari cha bei itakayo uzwa.

 chrispiny kalinga


Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking