Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma
kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya
watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa
mara ya kwanza katika mkutano wa tisa.
Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge
kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao
ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel
Ndumbaro kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida
Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido.
Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya
kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya
kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo
yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi.
Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu zitawasilisha taarifa zake Bungeni hapo.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking