Donderdag, Januarie 11, 2018

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKANUSHA YALE YALIYO TAPAKAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII.














MKUU WA MKOA WA NJOMBE 


Siku chache tu baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii sauti iliyodhaniwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akijadili namna ya utendaji wa Bunge na Awamu ya Tano ya Rais Magufuli mwenyewe ametolea ufafanuzi.

Akizungumza leo Jumatano Januari 10, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Longido, Sendeka amesema taarifa hiyo iliyoanza kusambaa tangu juzi inapaswa kupuuzwa.

Ameeleza kuwa sauti hiyo siyo ya kwake na kwamba imetengenezwa na kuongeza kwamba sauti hiyo imetengenezwa na wapinzani ili kumfarakanisha yeye na viongozi wa serikali na walio chini yao.

“… umahiri na heshima niliyoipata nchini na kwenye Bunge ni kubwa. Nilikwenda bungeni kutimiza wajibu kama mtuhumishi makini, sikwenda bungeni kuongeza idadi ya wabunge, nilikuwa mwakilishi nyinyi mnajua na Tanzania inajua"alisema.

Amesema vyama vya upinzani vimepata kiwewe na kuanza kumgombanisha na viongozi wa Serikali kwa kusambaza habari za uongo.

“Naomba mzipuuze habari hizi kwa kiwango kinachostahili kwani zote ni uzushi mtupu , badala yake elekezeni macho, fikra na mikakati yenu katika uchaguzi unaokuja.” Amesema RC Ole Sendeka.

Tayari Bunge kupitia kwa Spika Job Ndugai limemwandikia barua Ole Sendeka ili akahojiwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na kauli hiyo.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking