Woensdag, Januarie 31, 2018

LUDEWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI WAWAAMURU WANAFUNZI KWENDA KULIMA SHAMBA LA MWALIMU MUDA WA MASOMO.



 
Na chrispin kalinga. 
 
Walimu wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya lubonde shule ya msingi masimbwe wawaamrisha wanafunzi kwenda kulima shamba la mwalimu wa awali muda wa masoma.

wanafunzi wa shule ya masimbwe wamezungumza na waandishio wetu wa habari kwa kusema kuwa walimu hao wamekuwa na kawaida ya kuwaamrisha kwenda shamba kwanzia asubuhi saa moja hadi saa nne asubuhi kwenda kulima kwenye mashamba ya walimu wao.

wakaongeza kwa kusema kuwa wanafunzi wa darasa la saaba na darasa la sita sambamba na darasa la tano na la nne mara nyingi wao ndio huamrishwa kwa kwenda kufanya kazi ya shambani bila kuingia darasani kwa wakati.

wanafunzi hao wamezidi kuongea kwa kusema kuwa uongozi wa shule hiyo hauwatendei haki kwa kuwafanyisha kazi kwa muda wa masoma na si kuwafundisha na wamesema kuwa ufauru wao kwa mitiani ijayo wanawasiwasi kubwa kwa sababu mara nyingi wapo mashambani.

Na wakazidi kuiomba serikali kuingilia kati suara halo ili waweze kusoma na ufauli wao wa mtihani wa mwisho wa mwezi wa tisa mwaka huu uwe na ufauru mzuri ukilinganishwa na ufaulu ulio pita na wamesema kuwa wanaomba wazazi wao kupiga kelele kwenye uongozi wa shule hiyo kwa kuwaamrisha kwenda kulima kwenye mashamba ya walimu.

Njia  za kumtafuta msemaji wa shule hiyo yaani Mwalimu mkuu wa shule hiyo ziligonga mwamba na walimu wengine wakawaida waliwakimbia waandishi wetu wa habari .

Jitihada za kumtafuta kiongozi wa serikali katika kijijo hicho zoilifanyika na kumkuta afisa mtendaji wa kijiji hicho ndugu..ambaye naye alishikwa na mshangao kwa kuwaona wanafunzi mapema kiasi kile wakiwa wanalima katika shamba la mwalimu wa awali .

Afisa mtendaji huyo alidai kuwa alipo waona watoto hao wakilimishwa katika shamba hilo hakujua kuwa ni shamba la mwalimu na akaongeza kusema kuwa jambo la kuwalimisha wanafunzi kwenye shamba la walimu lipo nje kisheria  na taratibu za shule akaongeza kwa kusema kuwa hatua kali zinachuliwa dhidi ya uongozi na wasimamizi wa shule hiyo.








chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking