Dinsdag, Januarie 16, 2018


 Yaastahajabu ya Musa haya

Gari imeruka kutoka barabarani mpaka ghorofa ya pili California (picha+3)


Moja vitu ambavyo mataifa mengi yanapinga ni uendeshaji wa gari kwa mwendokasi kitu kinachosababisha kila kukicha kubuniwa mbinu za kudhibiti ajali sasa huko katika eneo la California gari lililokuwa linaendeshwa kwa kasi  liliruka na kuingia ndani ya ghorofa ya juu baada ya dereva wake kugonga uzio unaotenganisha ghorofa hilo na barabara.


Katika ajali hiyo sehemu moja ya gari ilibaki ikining’inia nje ya jengo hilo. Watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo walinusurika ila walipata majeraha madogo madogo, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.




















Polisi wamewaambia waandishi wa habari kuwa dereva wa gari hilo alikuwa ametoka hospitali na alikuwa anatumia dawa. Mmoja kati ya waliokuwepo kwenye gari alifanikiwa kujitoa ndani ya gari lakini mwingine alikwama kwa zaidi ya saa moja hadi maafisa wa uokoaji walipofika.

Ajali hiyo ilisababisha kuzuka kwa moto mdogo ambao zimamoto walifanikiwa kuuzima.
 

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking